Jumatano ya 6 ya Mwaka
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Mwa. 8:6 – 13, 20 – 22Ikawa mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikauka juu ya nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, naye akaona, na tazama, uso wa nchi umekauka.
Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akamtwaa katiak kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazini na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 116:12 – 15, 18 – 19Nitakutolea dhabihu ya kushukuru , ee Bwana.
Nimrudishie Bwana nini
Kwa ukarimu wake wote alionitendea?
Nitakipokea kikombe cha wokovu,
Na kulitangaza jina la Bwana.
K. Nitakutolea dhabihu ya kushukuru , ee Bwana.
Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana,
Naam, mbele ya watu wake wote.
Ina thamani machoni pa Bwana
Mauti ya wacha Mungu wake.
K. Nitakutolea dhabihu ya kushukuru , ee Bwana.
Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana,
Naam, mbele ya watu wake wote,
Katika nyua za nyumba ya Bwana,
Ndani yako, ee Yerusalemu.
K. Nitakutolea dhabihu ya kushukuru , ee Bwana.
Shangilio la Injili
Efe. 1:19 – 27Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ayatie nuru macho ya mioyo yetu, tujue tumaini la mwito wetu jinsi lilivyo.
Aleluya.
Injili
Mk. 8:22 – 26Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni