Jumatano. 30 Oktoba. 2024

Masomo ya Misa

Kumbukumbu ya Wat. Sirili (Mtawa) na Methodi (Asko (Jumanne, Februari 14, 2017)  

Somo la 1

Mwa. 6:5 – 8, 7:1 – 5, 10

Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analoliwaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana. Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki. Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, mume na mke. Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote. Kwa maana baada ya siku saba nitainyesha dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wan chi nitakifutilia mbali. Nuhu akafanya kama vile Bwana alivyomwamuru. Ikawa baada ya siku hizo saba, maji ya gharika yakawa juu ya nchi.

Wimbo wa Katikati

Zab. 29:1 – 4, 9 – 10

Sauti ya Bwana, enyi wana wa Mungu,
Mpeni Bwana utukufu na nguvu;
Mpeni Bwana utukufu wa jina lake;
Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.
(K) Bwana atawabariki watu wake kwa Amani.

Sauti ya Bwana I juu ya maji,
Bwana yu juu ya maji mengi
Sauti ya Bwana ina nguvu,
Sauti ya Bwana ina adhama.
(K) Bwana atawabariki watu wake kwa Amani.

Sauti ya Bwana yawazalisha ayala,
Na ndani ya hekalu lake wanasema wote, Utukufu.
Bwana aliketi juu ya Gharika;
Naam, Bwana ameketi hali ya mfalme milele.
(K) Bwana atawabariki watu wake kwa Amani.

Shangilio

Zab. 25:4 – 5

Aleluya, aleluya,
Ee Bwana, unijulishe njia zako, unifundishe mapito yako.
Aleluya.

Injili

Mk. 8:14 – 21

Wafuasi wake Yesu walisahau kuchukua mikate, wala chomboni hawana ila mkate mmoja tu. Akawaagiza, akasema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode. Wakabishana wao kwa wao, kwa kuwa hawana mikate. Naye Yesu akatambua, akawaambia, Mbona mnabishana kwa sababu hamna mikate? Hamfahamu bado, wala hamjaelewa? Je! Mioyo yenu ni mizito? Mna macho, hamwoni; mna masikio, hamsikii? Wala hamkumbuki? Nilipoivunja ile mikate mitano na kuwapa wale elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vimejaa vipande? Wakamwambia, Kumi na viwili. Na ile saba kuwapa wale elfu nne, mlichukua makanda mangapi yamejaa vipande? Wakamwambia, Saba. Akawaambia, Hamjafahamu bado?

Maoni


Ingia utoe maoni