Jumatatu ya 6 ya Mwaka
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Mwa. 4:1 – 15, 25Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoto na mtu asiye na kikao duniani. Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami niakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua. Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo yeyote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.
Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pia Habili; kwa sababu Kaini alimwua.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 50:1, 8, 16 – 17, 20 – 21Umtolee Mungu dhabihu za kushukuru.
Mungu, Mungu Bwana, amenena, ameiita nchi,
Toka maawio ya jua hata machweo yake.
Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako,
Na kafara zako ziko mbele zangu daima.
K. Umtolee Mungu dhabihu za kushukuru.
Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia,
Una nini wewe kuitangaza sheria yangu,
Na kuliweka agano langu kinywani mwako?
Maana wewe umechukia maonyo,
Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.
K. Umtolee Mungu dhabihu za kushukuru.
Umekaa na kumsengenya ndugu yako,
Na mwana wa mama yako umemsingizia.
Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza,
Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe.
Walakini nitakukemea;
Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.
K. Umtolee Mungu dhabihu za kushukuru.
Shangilio la Injili
1Sam. 3:9Nena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia: Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
Aleluya.
Injili
Mk. 8:11 – 13Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni