Jumamosi. 27 Aprili. 2024

Tafakari

Jumanne, Februari 14, 2017

Jumanne, Februari 14, 2017,
Juma la 6 la Mwaka wa Kanisa

Kumbukumbu ya Wat. Sirili (Mtawa) na Metodi (Askofu)

Mwa 6: 5-8; 7: 1-5, 10;
Zab 29: 1-4, 9-10;
Mk 8: 14-21.


CHACHU ULIMWENGUNI!

Kila anaye andaa mkate anatambua jinsi ya chachu kidogo (Amira) inavyo fanya kazi ndani ya donge la unga. Ukiweka kidogo tu ina umusha unga wote. Na yote hii inatokana tu na hii chachu kidogo tu. Kwahiyo ni nini hii chachu ya Mafarisayo na Herode? Ni maneno mabaya, maovu tena yenye makosa wanayo eneza. Kwa Mafarisayo, inaweza kuwa ni kushindwa kumwelewa Yesu alivyokuwa akifanya na kusema. Waliweza hata kubadilisha maneno yake kidogo tu na kuelezea kwa wengine katika maana tofauti. Hii ni mbaya sana na ilikuwa na madhara kwa kila mtu kwa wakati ule na baadae. Kidogo kidogo mbegu hiyo ndogo ya wasi wasi ingekuwa na kuenea kwa wengine.

Tunawaza kufikiria juu ya yote hayo, tukafahamu pia watu wanaofanya hivyo kwa wakati wetu. Lakini tunaweza kukosea kama hatujaanza kujiangalia sisi wenyewe kwanza. Je, ninafanya haya wakati mwingine? Je, nimejikuta nikipindisha ukweli kwa kutengeneza maneno ambayo huleta maana tofauti na jinsi mtu alivyosema? Je, ninawaongoza wengine kwa maneno ya uongo wakati naufahamu ukweli? Tunapaswa tuangalie maneno yetu na kutambua uzito uliopo katika maneno hayo. Maneno machache yaweza kuleta madhara makubwa kwa kipindi kikubwa. Ni vizuri kuwa na hali ya kupenda ukweli kwani kujaribu kupindisha ukweli huleta madhara makubwa daima.

Lakini pia sio hilo tu tunalopaswa kufanya. Tunapaswa kutambua pia neno dogo la upendo tunalosema limejaa utajiri mwingi ambao huweza kuleta mema na neema kwa muda wote. Pengine ni tabasamu tu dogo tunalo onesha au kitendo cha ukarimu ambacho tunadhani kinajiondokea tu bila kutambulika. Hili tabasamu dogo na ukarimu mdogo ni chachu ya Injili. Inaleta tofauti na kuleta chachu njema pia. Tutafakari juu ya mambo madogo tunayofanya katika maisha yetu. Tutambue kuwa labda iwe dhambi ndogo inaleta madhara makubwa , au kiwe kitendo kidogo cha upendo kinaleta Baraka kubwa mwishoni.

Sala: Bwana, nisaidie niweze kuwa mwaminifu na nisaidie niweze kutamua ni chachu ghani ninayo ileta katika maisha ya kila siku. Nisaidie niweze kujitenga na mabaya na unijaze mema. Nisaidie niweze kuwa chachu njema katika yote ninayo sema nakutenda kila siku. Yesu nakuamini wewe. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni