Jumatano. 30 Oktoba. 2024

Masomo ya Misa

Alhamisi ya 6 ya Mwaka (Alhamisi, Februari 16, 2017)  

Somo la 1

Mwa. 9:1 – 13

Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi. Kila mnyama nwa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani; pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu. Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyoawapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote. Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile. Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu. Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na wanadamu; maana kwa mkono wake Mungu alimfanya mwanadamu. Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake. Mungu akamwambia Nuhu, na wanawe pamoja naye, akisema, Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu; tena na kila kiumbe hai kilichopo pamoja nayi, ndege, kila mnyama wa kufugwa, na kil amnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi. Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo kuiharibu nchi. Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kil akiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele; Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.

Wimbo wa Katikati

Zab. 102:15 – 20, 28, 21 – 22

Mataifa wataliogopa jina la Bwana.
Na wafalme wote wa dunia utukufu wako;
Atakapoonekana katika utukufu wake,
Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa,
Asiyadharau maombi yao.
(K) Toka mbinguni Bwana ameiangalia nchi.

Kizazi kitakachokuja kitaandikiwa hayo,
Na watu watakaoubwa watamsifu Bwana.
Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu,
Toka mbinguni Bwana ameiangalia nchi
Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa,
Na kuwafungua walioandikiwa kufa.
(K) Toka mbinguni Bwana ameiangalia nchi.

Wana wa watumishi wako watakaa,
Na wazao wataimarishwa mbele zako.
Watu walitangaze jina la Bwana katika Sayuni,
Na sifa zake katika Yerusalemu.
Pindi mataifa watakapokusanyika pamoja,
Falme nazo ili kumtumikia Bwana.
(K) Toka mbinguni Bwana ameiangalia nchi.

Shangilio

Zab. 147:12, 15

Aleluya, aleluya,
Msifu Bwana, ee Yerusalemu, na neno lake nimelitumainia.
Aleluya.

Injili

Mk. 8:27 – 33

Siku ile Yesu alitoka na wanafunzi wake, wakaenda kwenye vijiji vya Kaisaria-Filipi; na njiani akawauliza wanafunzi wake, akasema, WAtu huninena mimi kuwa ni nani? Wakamjibu, Yohane Mbatizaji; wengine, Eliya; wengine, Mmojawapo wa manabii. Naye akawauliza, Na ninyi mnasema ya kuwa mimi ni nani? Petro akamjibu, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo. Akawaonya wasimwambie mtu habari zake. Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupatikana na mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka. Naye alikuwa akinena neno hilo waziwazi. Petro akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.

Maoni


Ingia utoe maoni