Jumatano. 30 Oktoba. 2024

Masomo ya Misa

Ijumaa ya 6 ya Mwaka (Ijumaa, Februari 17, 2017)  

Somo la 1

Mwa. 11:1 – 9

Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; ;wakakaa huko. Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala yam awe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilelel chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na hayo ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote.

Wimbo wa Katikati

Zab. 33:10 – 15

Bwana huyabatilisha mashauri ya mataifa,
Huyatangua makusudi ya watu.
Shauri la Bwana lasimama milele,
Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.
(K) Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.


Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao,
Watu aliowachagua kuwa urithi wake.
Toka mbinguni Bwana huchungulia,
Huwatazama wanadamu wote pia.
(K) Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.


Toka mahali pake aketipo,
Huwaangalia wote wakaao duniani.
Yeye aiumbaye mioyo yao wote
Huzifikiri kazi zao zote.
(K) Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.

Shangilio

Zab. 119:13

Aleluya, aleluya,
Umwangazie mtumishi wako uso wako, na kunifundihsa amri zako.
Aleluya.

Injili

Mk. 8:34 – 9:1

Yesu aliwaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha. Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe ini badala ya nafsi yake? Maana kil amtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu. Akawaambia, Amin, nawaambia, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.

Maoni


Ingia utoe maoni