Jumapili. 28 Aprili. 2024

Tafakari

Jumatano, Februari 15, 2017

Jumatano, Februari 15, 2017,
Juma la 6 la Mwaka wa Kanisa

Mwa 8: 6-13, 20-22;
Zab 116: 12-15, 18-19;
Mk 8: 22-26.


HATUA MOJA MBELE!

Daima, mara nyingi katika Injili Yesu anapo mponya mtu, inakuwa ni kwasababu ya imani walio onesha. Si kwamba Yesu hakuweza kumponya mtu bila imani, bali, ndivyo hivi alivyopenda kutenda. Alifanya uponyaji akiegemea kwenye imani kamili. Katika habari ya muujiza wa leo, Yesu anafanya kitu kingine kinachosema sana. Anaruhusu mtu aponywe kwa kiasi tu ili aweze kuelezea juu ya uhaba wa imani yake. Lakini anataka kutufunulia pia sisi kwamba imani kidogo yaweza kutupeleka kwenye imani kubwa. Huyu mtu alikuwa anaweza kuona kidogo tu, taratibu akaanza kuamini zaidi. Na hatimaye imani yake ikakuwa, Yesu ananyoosha mkono wake juu yake nakumalizia uponyaji wake katika ukamilifu wote.

Ni jambo lilokubwa kwetu la kujifunza! Baadhi ya watu wanaweza kuwa na imani kamili kwa Mungu na vitu vyote. Kama huyo mtu ni wewe, kwa kweli umebarikiwa. Lakini pia ujumbe huu unalenga wale ambao wana imani lakini daima wanakazana kuikamilisha. Wanao anguka katika msafara huu, Yesu anatoa tumaini kubwa zaidi. Kitendo cha kumponya huyu mtu mara mbili, kina tueleza kwamba Yesu ni mvumilivu na mwenye huruma na atachukua kidogo tulicho nacho, na kidogo tunachompa, na kukitumia katika hali ya ukamilifu apendavyo. Atafanya kazi kubadili imani yetu ndogo ili sisi tuweze kupanda ngazi moja tena mbele kumwelekea Mungu na kukua katika imani.

Katika hali ya dhambi pia. Wakati mwingine tuna huzuni kidogo sana juu ya dhambi tunazo tenda, hata kama tunajua ni mbaya. Kama huyo mtu ni wewe, jaribu kuchukua hatua moja mbele kutafuta uponyaji na msamaha. Jaribu, kutamani hilo na utakuwa katika hali ya kujuta dhambi. Hali hii inaweza ikawa kidogo sana, lakini ukionesha jitihada kidogo Yesu atakusaidia na kukufanya mwema kabisa usiye penda dhambi.

Tumwagalie huyu mtu aliyekuwa kipofu na hali yake ya kuponywa na kuongoka. Fanya hili tendo ni wewe na tambua Yesu anataka kukupeleka hatua moja mbele kumwelekea yeye katika imani na katika maungamo yako ya dhambi.

Sala: Bwana, ninakushukuru kwa uvumilivu wa ajabu ulionao juu yangu. Ninajua imani yangu juu yako ni kidogo naomba uiongeze. Bwana ninakuomba uchukue imani kidogo nilio nayo na majuto kidogo nilio nayo kwasababu ya dhambi zangu yatumie kunipeleka hatua moja mbele tena kukuelekea wewe na Moyo wako wa huruma. Yesu nakuamini wewe. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni