SHEREHE YA KUZALIWA MTAKATIFU YOHANE MBATIZAJI
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Isa 49:1-6Akaniambia; Wewe u mtumishi wangu, Israeli, ambaye katika wewe nitatukuzwa. Lakini nikasema. Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina Bwana, na thawabu yangu ina Mungu wangu.
Na sasa Bwana asema hivi, yeye aliyeniumba tangu tumboni niwe mtumishi wake, ili nimletee Yakobo tena. na Israeli wakusanyike mbele zake tena; (maana mimi nimepata heshima mbele ya macho ya Bwana, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu); naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo. na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 139:1-3, 13-15Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa.
Ee Bwana umenichunguza na kunijua.
Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu;
Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu,
Umeelewa na njia zangu zote.
K. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa.
Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu,
Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa
Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha.
Matendo yako ni ya ajabu.
K. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa.
Na nafsi yangu yajua sana,
Mifupa yangu haikusitirika kwako,
Nilipoumbwa kwa siri,
Nilipoungwa kwa ustadi
pande za chini za nchi.
K. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa.
Somo la Pili
Mdo. 13 : 22-26Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Lk. 1 : 76Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake aliye juu. Utatangulia mbele za uso wa Bwana, umtengenezee njia zake.
Aleluya.
Injili
Lk. 1 : 57-66, 30Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni