Jumatano. 15 Mei. 2024

Tafakari

Jumamosi, Juni 24, 2017


Jumamosi, Juni 24, 2017.
Juma la 11 la Mwaka wa Kanisa

Sherehe ya kuzaliwa kwa Mt.Yohane Mbatizaji

Is 49: 1-6;
Zab 138: 1-3, 13-15;
Mdo13: 22-26;
Lk 1: 57-66, 80


ISHARA YA UTUKUFU YA JUA LA HAKI !

Kwa kawaida Kanisa alisheherekei sikukuu za kuzaliwa za watakatifu. Lakini kuna sikukuu nyingine za pekee ambazo ni kuzwaliwa Bwana wetu Yesu Kristo-na sherehe za kuzaliwa Bikira Maria naya kuzawaliwa kwa Yohane mbatizaji. Hii ni kwasababu Maria, tangu kuumbwa kwake kwanza alikingiwa dhambi ya asili. Yohane Mbatizaji alitakaswa kutoka dhambi ya asili akiwa tumboni mwa mama yake. Leo inajulikana kama “Noeli ndogo” kwasababu Yohane alimtangulia Yesu na alimbatiza Kristo. Maisha ya Yohane Mbatizaji yalijazwa na jambo moja-kumuonesha Yesu kwa watu na kuandaa ujio wa Ufalme wa Mungu. Maandiko matakatifu yanatuambia kwamba Yohane Mbatizaji alijazwa na Roho Mtakatifu hata angali tumboni mwa mama yake (Lk 1: 15, 41) na Kristo mwenyewe ambaye Bikira Maria alipata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Moto wa Roho Mtakatifu ulimjaza Yohane na akawa mtangulizi wa Masiha. Yohane alivunja ukimya wa manabii wa karne zilizopita alipoanza kuongelea kuhusu Neno wa Mungu kwa watu wa Israeli. Akiwa katikati ya watu waliopoteza matumaini yao kuhusu Mungu, sasa anaiamsha tena Imani yao, kuwatahadharisha kuhusu usafi wa mioyo yao, kuamsha tena ndani yao mapenzi mema ya kumtambua na kumkubali Masiha anayekuja. Watu walikimbilia jangwani kwenda kumsikiliza na kubatizwa.

Yohane aliitwa kutoka tumboni mwa mama yake kuwa mjumbe wa ufalme wa Mungu. Kwa njia hiyo hiyo Yesu naye anatualika sisi tuliowafuasi wake na tuliobatizwa kwa jina lake, tuweze kuwa manabii- tuwe watu wanaotangaza kwa maneno na matendo ujumbe wa haki na huruma. Tangu ubatizo wetu (Kuzaliwa katika maisha ya Kimungu) sisi kama Yohane, tuna utume wakufanya kutoka katika mpango wa Baba yetu. Sio tuu kumfuata Yesu, bali kutangaza siku ya ukombozi tunayo tumaini ndani ya kristo kwamba itatimilizwa.

Tutafakari leo, hasa katika zile hali ambazo hatukuwa waaminifu kwa Mungu katika maisha yetu. Mungu atatupokea tena na kubadilisha maisha yetu. Mungu anatusubiri na huruma yake haina kikomo. Turuhusu huruma yake ijaze mioyo yetu ili iweze kupokea daima uzuri wa Mungu. Nasi pia kama Yohane, alivyo itwa kuwa mjumbe wa Ufalme wa Mungu, Yesu anampa kila mbatizwa Roho wake kutangaza kwa maneno na matendo ufalme wa haki na huruma.

Sala: Bwana, nisaidie niweze kuona dhambi zangu za zamani si katika hali ya kupoteza tumaini bali kama sababu ya kurudi kwako kwa uaminifu mkubwa. Bila kujali nimeanguka mara ngapi, nisaidie niweze kunyanyuka na kuimba tena sifa zako. Yesu nakuamini wewe. Mt. Yohane mbatizaji mhubiri wa ukweli usiye kuwa na woga, utuombee. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni