Jumanne ya 11 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
2 Kor. 8:1 – 9Hata tukamwonya Tito kuwatimilizia neema hii kwenu kama vile yeye alivyotangulia kuianzisha. Lakini kama mlivyo na wingi wa mambo yote; imani, na usemi, na elimu, na bidii yote, na upendo wenu kwetu sisi; basi vivyo hivyo mpate wingi wa neema hii pia. Sineni ili kuwaamuru, bali kwa bidii ya watu wengine nijaribu unyofu wa upendo wenu. Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 146:2, 5 – 9Ee nafsi yuangu, umsifu Bwana.
Ee nafsi yangu umsifu Bwana
Nitamsifu Bwana muda ninaoishi,
Nitamwimbia Mungu wangu ningali hai.
K. Ee nafsi yuangu, umsifu Bwana.
Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,
Na tumaini lake ni kwa Bwana, Mungu wake,
Aliyezifanya mbingu na nchi,
Bahari na vitu vyote vilivyomo.
K. Ee nafsi yuangu, umsifu Bwana.
Huishika kweli milele,
Huwafanyia hukumu walioonewa,
Huwapa wenye njaa chakula,
Bwana hufungua waliofungwa.
K. Ee nafsi yuangu, umsifu Bwana.
Bwana huwafumbua macho waliopofuka,
Bwana huwainua walioinama,
Bwana huwapenda wenye haki
Bwana huwahifadhi wageni,
Huwategemeza yatima na mjane.
K. Ee nafsi yuangu, umsifu Bwana.
Shangilio la Injili
Ebr. 4:12Neno la Mungu li hai tena li na nguvu, li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Aleluya.
Injili
Mt. 5:43 – 48Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni