Jumanne ya 8 ya Mwaka
· Mwaka A
Somo la Kwanza
YbS. 35 : 1-12Umheshimu Bwana kwa jicho la ukarimu, wala usimtolee malimbuko ya kazi za mikono yako kwa ubahili. Kwa kila kitolewacho uonyeshe ukunjufu wa uso, hata sehemu ya kumi uiweke wakfu kwa changamko. Mpe Mungu kama alivyokupa wewe; na kama mkono wako ulivyopata, utoe kwa ukarimu. Amhurumiaye maskini humkopesha Bwana, naye ni nani awezaye kulipa isipokuwa ni yeye; kwa kuwa Bwana hulipa, naye atakulipa wewe mara saba.
Usidhanie kuwa unaweza kutoa rushwa, kwa maana Yeye hazipokei; wala usiwaze moyoni kutoa dhabihu ya jeuri, kwa kuwa Bwana ndiya mhukumu wala hakijali cheo cha mtu.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 50 : 5-8, 14, 23Nitamwonyesha wokovu wa Mungu autengenezaye mwenendo wake.
Nikusanyieni wacha Mungu wangu
Waliofanya agano nami kwa dhabihu.
Na mbingu zitatangaza haki yake,
Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.
K. Nitamwonyesha wokovu wa Mungu autengenezaye mwenendo wake.
Sikieni, enyi watu wangu, nami nitanena,
Mimi nitakushuhudia, Israeli;
Mimi ndimi niliye Mungu, Mungu wako.
Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako,
Na kafara zako ziko mbele zangu daima.
K. Nitamwonyesha wokovu wa Mungu autengenezaye mwenendo wake.
Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru,
Mtimizie Aliye iuu nadhiri zako.
Atoaye dhabihu za kushukuru,
Ndiye anayenitukuza.
Naye autengenezaye mwenendo wake,
Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.
K. Nitamwonyesha wokovu wa Mungu autengenezaye mwenendo wake.
Shangilio la Injili
LK 8:15Injili
Mk. 10:28-31Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni