Jumatatu. 13 Mei. 2024

Tafakari

Jumanne, Februari 28, 2017

Jumanne, Februari 28, 2017,
Juma la 8 la mwaka wa Kanisa

YbS 35: 1-12;
Zab 50: 5-8;
Mk 10: 28-31.


KUMFUATA YESU BILA MASHARTI!

Baadhi wameitwa kuacha mengi na kumfuata Yesu. Baadhi ya hawa wameitwa kuishi maisha ya kitawa (wakike na wakiume). Wanaacha yote ya ulimwengu na kufuata mwaliko wa Yesu wa kumfuata katika hali ya pekee. Sisi wote lakini tumeitwa “kuacha yote” na kumfuata Yesu katika hali zetu za kipekee. Kwa kuacha yote, tunaitwa kukabidhi yote, uhuru wetu na kutumikia kwa kadiri ya mpango mtakatifu wa Kristo. Hili linaweza likachukua hali mbali mbali lakini mwishoni, linahitaji daima kuacha yote.

Habari njema ni kwamba ‘kuacha yote’ si zaidi ya kuacha mitazamo yetu mibaya ya maisha na kuchagua mapenzi ya Mungu. Maisha alio tuandalia ni mazuri kuliko hata chochote tunachoweza kufikiri. Kwa kusema “hapana” kwa mapenzi yetu na kufanya vitu kwa njia zetu, ni wazi tunasema “Ndio” kufanya vitu kwa ukamilifu wa Kimungu. Hata iwe ni wito ghani wa pekee katika maisha yako, ni vizuri kukumbatia mapenzi ya Mungu.

Tutafakari ni namna ghani mimi na wewe tupo tayari kusema “ndio” kwa Yesu bila kujali anatutaka nini. Je, upo tayari kusema ndio hata kwa kile ambacho hajakufunulia bado? Sema “ndio” leo kwa maisha yako ya baadae na Mungu atakujaza Baraka katika njia hiyo.

Sala: Bwana, haijalishi ni nini umeniitia kufanya katika maisha, jibu langu ni “ndio”. Ninataka kukutumikia kwa moyo wote. Nisaidie niweze kuishi wito huo kwa ukarimu na mapendo. Yesu, nakuamini wewe. Amina!

Maoni


Ingia utoe maoni