Jumatatu ya 7 ya Mwaka
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Ybs. 1:1 – 10Hekima iliumbwa kabla ya vitu vyote, na ufahamu wa busara tangu milele. Nani aliyefunuliwa shina la hekima? Nani aliyejua mashauri yake merevu?
Yuko mmoja aliye na hekima, naye yu wa kuogopwa sana, ameketi katika kiti chake cha enzi.
Bwana ndiye aliyeiumba na kuiona na kuihesabu, na kumwaga juu ya kazi zake zote. Ina wote wenye mwili kama aitoavyo, na wale wampendao amewapa kwa wingi.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 93:1 – 2, 5Bwana ametamalaki, amejivika adhama.
Bwana ametamalaki, amejivika adhama,
Bwana amejivika, na kujikaza nguvu.
K. Bwana ametamalaki, amejivika adhama.
Naam, ulimwengu umethibitika isitikisike;
Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani;
Wewe ndiwe uliye tangu milele.
K. Bwana ametamalaki, amejivika adhama.
Shuhuda zako ni amini sana;
Utakatifu ndio uifaao nyumba yako,
Ee Bwana, milele na milele.
K. Bwana ametamalaki, amejivika adhama.
Shangilio la Injili
Zab. 27:11Ee Bwana, unifundishe njia yako, na kuniongoza katika njia iliyonyoka.
Aleluya.
Injili
Mk. 9:14-29Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini; akagaagaa. Akitokwa na povu. Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, tangu utoto. Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwamngamize; lakini ukiweza neno lolote, utuhurumie, na kutusaidia. Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu. Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena. Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa. Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua; naye akasimama.
Hata alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa? Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lolote, isipokuwa kwa kuomba.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni