Jumanne ya 9 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Tob 2:9–14Basi mke wangu Ana alikuwa akifanya kazi ya kusokota vyumbani mwa wanawake, naye alipokwisha kazi huzipeleka kwao wenyewe. Wao wakamlipa mshahara; tena wakampa na zawadi ya mwanambuzi. Na yule mwanambuzi alipokuwamo nyumbani mwangu alianza kulia. Kwa hiyo nikamwuliza mke wangu, Huyu mwanambuzi ametokapi? Je! Hukumwiba? Uwarudishie wenyewe, maana si halali kula kilichoibiwa. Naye akanijibu, A-a, ni zawadi yangu niliyopewa faida zaidi ya mshahara wangu, Lakini mimi sikumsadiki; nikamwagiza awarudishie wenyewe; nikamwonea haya. Akarudisha maneno, Je! Wewe, zi wapi basi sadaka zako na matendo yako ya haki? Tazama ati! Umefahamika wewe na kazi zako zote.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 112:1-2, 7-9Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana.
Aleluya.
Heri mtu yule amchaye Bwana,
Apendezwaye sana na maagizo yake.
Wazao wake watakuwa hodari duniani;
Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.
K. Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana.
Au: Aleluya.
Hataogopa habari mbaya;
Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana.
Moyo wake umethibitika hataogopa.
Hata awaone watesi wake wameshindwa.
K. Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana.
Au: Aleluya.
Amekirimu, na kuwapa maskini,
Haki yake yakaa milele,
Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.
K. Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana.
Au: Aleluya.
Shangilio la Injili
Zab 147:12, 15Msifu Bwana, Ee Yerusalemu, huipeleka amri yake juu ya nchi.
Aleluya.
Injili
Mk 12:13-17Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni