Jumatatu, Julai 08, 2024
Jumatatu, Julai, 8, 2024,
Tafakari ya kila siku
Juma la 14 la Mwaka wa Kanisa
Hos 2: 16-18, 21-22;
Zab 144: 2-9;
Mt 9: 18-26
UPONYAJI WA IMANI!
Leo katika Injili, tunaona matukio mawili ya miujiza wa kuponya. Hawa ni watu walio muhitaji Yesu ili waponywe. Tunakutana na watu wengi wanao ulizia kuhusu upendo wa Mungu na kwanini Mungu hawaponyi? Kuna wengine pia wanajiuliza pia kuhusu Imani yao wenyewe wanajisikia kama wangekuwa na Imani kubwa zaidi kwa Mungu ungekuta Mungu amesha waponya.
Kijana mmoja aliitwa Stefano wa umri wa miaka 18, alipata ajali ya gari na alipata hitilafu katika ubongo wake kiasi cha kushindwa pia kuongea vizuri. Na mwaka mmoja baadaye akadondoka kutoka kwenye paa la nyumba, akapooza kuanzia kwenye kiuno kushuka chini. Daktari akamwambia Stefano hutaweze kutembea tena. Lakini Stefano akamwambia Mungu ameniambia huu ni muda wake wakuniponya. Imani yake ilikuwa ya kweli na hakika, hakuwa na mashaka yeyote kwamba Mungu atamponya. Siku moja watu walikusanyika kumuombea, yeye alienda mbele kwakujivuta na kukaa mbele yao, wakamuombea na kusali sana lakini hali yake ikabaki vile vile. Baada ya hapo watu walimuhuzunikia sana kwa hali yake. Walishangaa sana kwamba alikuwa na Imani na walijiridhisha kwamba atapona lakini wakashangaa sasa Imani yake imekuwaje tena? Baada ya mkutano wao wakamkuta Stefano wakashngaa. Alikuwa hayupo vizuri lakini Imani yake ilikuwa haijayumbishwa. Kwa sauti ya huzuni Stefano alisema “haikuwa muda wangu wakupona lakini siku moja nitasimama na kukimbia”.
Hakika tuna muujiza hapa. Muujiza haukuwa katika miguu yake, bali ulikuwa muujiza wa roho yake. Mwanga wa Yesu ulikuwa ukingaa ndani ya roho yake. Na zaidi ya yote, uponyaji wa mwili ni kwa ajili ya muda mfupi. Bali uponyaji wa roho na Uponyaji wa Imani unadumu kwa ajili ya uzima wa milele. Tumuombe Mungu atusaidie kushughulika zaidi na uponyaji wa Imani yetu na maisha yetu ya kiroho ili tuweze kupata nafasi katika maisha ya milele.
Sala:
Bwana naomba uniponye kiroho.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni