Ruka hadi maudhui
Mkatoliki Leo
Tafakari

Tafakari ya Jumapili, 15 Oktoba 2023

· na Shajara Administrator

Masomo ya siku hii Dominika ya 28 ya Mwaka → Isa 25:6-10 · Zab 23 · Flp 4:12-14, 19-20 · Mt 22:1-14
ambacho mtu anakipigania na kukitafuta bali ni kupokea kama zawadi kutoka kwa Mungu, na Mwanae Yesu. Lakini pia maana ya karamu inabadilishwa pia katika hali ya karamu ya mwisho ya Mwana kondoo ambapo hukumu itakuwa kwa Waisraeli. Hawa ni wale watakao hukumiwa kwa kutokupokea ufalme huu wa Mungu kwa njia ya Mwanae Yesu Kristo. Maada hii inaendelea pia katika jumuiya ya waumini ambao wamepokea ufalme wa Mungu. Hivyo ufalme wa Mungu, ingawaje ni zawadi kwetu, inahitaji mwitikio. Kukubali hili inabidi kuacha maisha ya zamani na kumvaa Kristo kwa maisha mapya au kwa namna nyingine tuvae utu wa Mungu. Kukubaliwa kwetu na Mungu inatagemea sana jinsi tulivyokubali Ufalme wake. Wakati Mungu alivyo niita mimi kumfuata, napaswa kumfuata na kujibu wito wake bila kujibakiza.

Sala:
Bwana, ninakupa wewe maisha yangu. Ninaomba niweze kuwa muwazi kwako kila siku kwa kila njia, nikitafuta kupokea kila neno linalo tumwa kutoka katika moyo wako wa huruma. Ninakuomba nitumiwe nawe niweze kuwa chombo cha huruma kwa watu wote ulimwenguni. Yesu nakuamini wewe.
Amina
0 Maoni
WhatsApp Facebook

Maoni (0)

Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.

Ingia utoe maoni