Ijumaa, Septemba 15, 2023
Ijumaa, Septemba 15, 2023
Juma la 23 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu ya Bikira Maria Mtakatifu wa Mateso
Ebr 5: 7-9; au 1Kor 15:1-11
Zab 30: 2-6, 15-16, 20;
Yn 19: 25-27, 35 au Lk 2: 33-35
KUTESEKA KWA AMANI NA FURAHA!
Leo tunakumbuka mateso ya Mama yetu Bikira Maria. Mateso ya Maria yalikuwa ya ndani. Bikira Maria alikuwa mwanadamu kamili kwasababu hakutenda dhambi na kati ya watu waliompendeza Mungu katika hali ya ukamilifu wote ni Bikira Maria licha ya Mwanae, lakini kwa ajili ya hili hatuwezi kusema hakuwa na hisia ya kuhisi mambo ya duniani. Kwasababu ya ukamilifu wake, alipenda kwa mapendo ya ndani kuliko sisi. Kwasababu ya upendo huu, alihisi uchungu wa kumpoteza mwanae kuliko sisi. Mateso ya Maria tofauti na yetu yalikuwa kamili. Mateso yetu mara nyingi yamechanganyika na udhaifu wetu. Maria hakuhuzunika kwasababu atamkosa Mwanae ampe msaada. Aliteseka kwasababu aliona mateso ya yule anaye mpenda, na akahisi mateso yale kama Mwanae alivyohisi. Tunaweza kuhisi pia ni kwa jinsi ghani Yesu alivyojisikia alivyomuona Mamaye katika huzuni. Ni hakika ilimsababishia mateso pia, lakini ilikuwa pia ni hali ya kuonesha ukaribu wao. Ulimwengu mzima unaweza kuwa umekuwa wa ukatili na hali zote, lakini uso wa Mama yake ulikuwa ni sehemu pekee alioweza kuelekezea macho yake, akiona sura na mfano aliouweka wakati anatuumba sisi.
Huzuni ya mama haikuwa ni huzuni bila matumaini. Alijua kwa matumani fulani kwamba Mwanae atafufuka kutoka wafu. Tumaini lake halikumzuia kuhisi uchungu na wala halikumzuia kutazamia ufufuko wake. Maria ni Mama yetu. Kama ilivyo kwa Mama mwema, anatufundisha sisi. Tunapaswa tutuoe muda wetu tukiwa naye katika mti wa Msalaba, tukimuomba atufundishe jinsi ya kuhisi nasi mateso yetu katika maisha. Tusisite kumkimbilia atuombee tunapokumbana na adha na mateso katika maisha, yeye awe faraja na msaada wetu kwani atakuwa nasi, akisimama nasi na kuteseka nasi, akiyaweka yote chini ya Msalaba wa Mwanae kwa niaba yetu.
Sala:
Mama wa Upendo, Mama wa Mateso na Mama wa huruma, utuombee sisi.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni