Ruka hadi maudhui
Mkatoliki Leo
Tafakari

Upendo wa Kweli Unaondoa Hofu

· na Shajara Administrator

Masomo ya siku hii Ijumaa ya 34 ya Mwaka → Ufu 20:1-4, 11-21:2 · Zab 84:2-5, 7 · Lk 21:29-33
Katika Injili ya leo, Yesu anatuambia sisi kwamba kama tunamjua Mungu, tutatambua lengo lake, na tamaa yake juu yetu. Matokeo yake, kama tunavyo elewa kipindi cha mavuno kimekaribia, tutakuwa tayari kusoma alama za nyakati, na wakati wa mwisho utakapo karibia, tutakuwa tayari, kwasababu tutakuwa tumeshalindwa na mawazo kwamba hakuna kiwezacho kututenga na upendo wa Mungu, si wala mwisho wa nyakati/dunia. Yesu alisema “mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayata pita kamwe”, Na maneno ya Mungu ni “nawapenda” hivyo hakuna cha kuogopa tukibaki katika pendo la Mungu daima.

Sala:
Naomba nijengwa katika mizizi ya Upendo wako Ee Bwana.
Amina
0 Maoni
WhatsApp Facebook

Maoni (0)

Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.

Ingia utoe maoni