Ijumaa. 22 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Disemba 10, 2016

Jumamosi, Desemba 10, 2016,
Juma la 2 la Majilio

YbS 48: 1-4, 9-11;
Zab 79: 2-3, 15-16, 18-19;
Mt 17: 10-13


KUKUBALI KUTUBU

Kazi ya Yohane Mbatizaji kama Elisha aliyekuja Waandishi walishindwa kuiona. Walishindwa kumuona yeye akitimiza kazi ya Elisha ya kuandaa njia kwa ajili ya Bwana. Kama Yohane alivyokuwa na kazi ya pekee ya kumtambulisha na kuandaa njia kwa ajili ya ujio wa Kristo, sisi pia tuna kazi ya kumkaribisha Yesu daima. Yesu alikuja miaka mingi iliopita, lakini daima anatamani kuja daima katika maisha yetu. Na anaweza kuja tu kama tumejiandaa vizuri.

Ujumbe mkuu wa Yohane ni kutubu dhambi zetu. Ingawaje sisi wote tunakazana kujikinga na dhambi, kwasababu ya matokeo ya kuanguka kwa Mwanadamu, hatupaswi kusahau kwamba wito wetu ni kuwa wakamilifu, kuwa wakamilifu kama Baba yetu wa Mbinguni alivyo mkamilifu. Tunaitwa kutambua dhambi zetu, kuziungama, na kujitahidi kujinasua kutoka kwenye dhambi hizo.

Kipindi cha majilio ni kipindi muhimu cha kufanya hivyo daima, na ni muhimu kutafuta neema zinazopatikana kwa neema ya Sakramenti ya kitubio katika kipindi hiki kitakatifu. Tujitazame wenyewe katika mioyo yetu ni kwa jinsi ghani tulivyo tayari kuihubiria mioyo yetu kuhusu kutubu na kuacha dhambi. Kukubali toba kutubu kipindi hiki ni kitu chema kabisa ambacho twaweza kufanya ili kuandaa kuja kwa Kristo daima katika maisha yetu.

Sala: Bwana, nisaidie niweze kuziona dhambi zangu kadiri tunavyozama katika kipindi hichi cha majilio. Nisaidie niweze kutambua yale yote yanayonifanya niwe mbali nawe na kuyaacha kwa moyo wote. Yesu nakuamini wewe. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni