Jumapili, Mei 17, 2020
Jumapili, Mei 17, 2020.
Dominika ya 6 ya Pasaka
Mdo 8: 5-8, 14-17;
Zab 65: 1-7, 16, 20;
1 Pet 3: 15-18;
Yn 14: 15-21.
ROHO MTAKATIFU, MSAIDIZI!
Kwa, jumapili ya sita ya Pasaka tunaanza kufungua macho yetu na kuanza kutazamia ujio wa Roho Mtakatifu. Yesu anaongea kuhusu kumuomba Baba alete msaidizi mwingine awe nasi daima. Huyu msaidizi ni Roho Mtakatifu.
Katika somo la kwanza tunasikia kuhusu Filipo. Anafika Samaria na anaanza kuhubiri Injili na kubatiza wote waliopokea Imani. Roho Mtakatifu aliwaimarisha wamisionari hawa wa kwanza kwa kuwapa nguvu katika maneno yao kwa kudhihirisha uwepo wake kwa ishara. Watu wa mji ule walibadilika na wakajazwa na furaha. Sehemu ya pili ya somo inamuonesha Petro na Yohane wakiwatembelea wabatizwa huko Samaria. Mitume hawa wawili waliwawekea mikono ili Roho Mtakatifu aweze kuwa juu yao. Walishangazwa Wasamaria waliobatizwa na Filipo walikuwa hawajapokea Roho Mtakatifu. Uwepo wa Mungu ulikosa ishara ya njee ambayo ilikuwepo wakati wa Kanisa la mwanzo. Luka anaunganisha matukio haya mawili, kutuonesha kwamba kila sehemu Injili ilipo hubiriwa kuna jumuiya mpya inayokuwa. Lakini, hawakuhitaji kukuwa, kuendelea na kuishi katika hali ya pekee kabisa na inayo jitegemea. Ni vizuri walianzisha umoja wa kuunganisha na kanisa nzima. Ni Roho pekee atakaye jidhihirisha ndani yao wote.
Katika somo la Injili tunaona ujumbe wa wosia wa Yesu. Mitume wanahuzuni kwababu ya kuondoka kwa Yesu, na wana ahidiwa msaidizi mwingine Yesu anaeleza wazi kwamba Roho Mtakatifu watampokea tu wale waIe walioungana naye, katika mipango yake na katika kazi zake za upendo. Huyu Roho anaitwa kwa majina mawili. Mfariji na Roho wa kweli.
Msaidizi ni neno linalo onesha kwamba ni yule aliyeitwa ili aweze kuambatana. Hapo kale kulikuwa hamna kuanzishwa kwa sheria, kila mtu alipaswa kujitetea na kujilinda mwenyewe. Ilitokea mara chache kwamba, mtu hana kosa, lakini mtu haweze kudhihirisha kwamba hana hatia. Kwake kilicho salia ni tumaini moja tu: kwamba mtu mmoja wa heshima atatokea katika mkutano aongee bila kusita na kutoa ushahidi wa kumtetea. Ishara hii ni sawa na kufunguliwa gerezani. Na wala hakuna yeyote atakaye kushutumu tena. Huyu anaitwa “Msaidizi” maana yake yule anayeitwa ili aweze kuwa karibu na mwingine ambaye amepata matatizo. Yesu aliwahidia wafuasi wake msaidizi, kwasababu tayari wamesha mpata wa kwanza ambaye ni Yesu mwenyewe. Roho Mtakatifu ni Msaidizi kwasababu anawasaidia Wafuasi katika vita dhidi ya malimwengu hasa maovu. Yohane anawakumbusha wafuasi juu ya ukweli huu ili wanapo kutana na ugumu katika maisha, wasikatishwe tamaa, kupoteza tumaini, bila kupoteza Amani ya moyo na furaha. Wafuasi waliamini juu ya usaidizi wa Roho Mtakatifu. Wana amini nguvu ya Msaidizi huyu na kwamba hatashindwa.
Roho wa ukweli anafanya kazi katika huduma ya kweli. Ujumbe wa Yesu umeelekezwa kwa watu wote. Unapaswa kuhubiriwa mpaka miisho ya ulimwengu. Roho Mtakatifu anadhihirisha kwamba hatashindwa, na wala hayata fafanuliwa vibaya na kuharibiwa, mafundihso ya Kristo. Yeye haondoi tu makosa yanayo fanywa na kukosewa katika kurithisha ujumbe wa Yesu. Anawatambulisha wafuasi katika ukweli wote. Yeye yupo katika kuwaelekeza wafuasi katika kutambua ukweli wote. Hatasema kitu kingine kipya kinacho pinga ujumbe wa Yesu. Atasaidia katika kuendeleza ujumbe wa Yesu mpaka miisho yote. Kazi ya Wakristo nikubaki imara katika kazi hii ya Roho Mtakatifu ambaye daima anafunua mambo mapya. Yeye kwa asili ndiye anaye ufanya upya uso wa Nchi (104:30). Ni dhambi juu ya Roho Mtakatifu kupinga kufanywa upya, kukataa kufanya mabadiliko katika maisha ya jumuiya, ambayo yanawaleta watu karibu na Yesu na wandugu, ambayo huongeza furaha na amani ambayo yanawafanya watu wasali vizuri na kufanya moyo uwe huru na kuondoa hofu zote.
Kama tupo wazi kwa ujio wa Roho Mtakatifu, tutapokea Msaidizi mzuri kabisa katika maisha yetu yote. Roho Mtakatifu ndiye msaidizi tunaye mhitaji. Kuzama ndani ya Roho Mtakatifu inatufanya tujazwe na neema zote katika maisha. Sali sala ya Roho Mtakatifu na kutarajia kusherekea dominika ya Pentekoste jumapili mbili zijazo.
Sala:
Ee, Mungu, wewe ambaye kwa Roho Mtakatifu, unaongoza Roho za Waamini wako, jalia kwa Roho huyo huyo, tuweze kuwa wakweli na wenye hekima na kufurahia faraja yake, kwa Njia ya Kristo Bwana wetu. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni