Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Januari 09, 2020

Alhamisi, Januari 9, 2020.
Juma baada ya Epifania

1 Yoh 4:19 - 5:4;
Zab 72: 1-2, 14-15;
Lk 4: 14-22

YESU, MASIHI WETU!

Leo, Yesu akiwa katika Sinagogi anasoma kutoka kitabu cha nabii Isaya Ndani ya Yesu tunaona neema ya Mungu ikifanya kazi kwa vitendo. Maneno yake yanaleta matumaini, furaha, na neema
kwa wale wote walio tayari kumpokea. Tangazo lake la kutimiza unabii wa Masiha aliotangaza nabii Isaya unaleta mshangao kwa watu wa kijiji chake.

Isaya alikuwa ametabiri kwamba Masihi atakuja katika nguvu ya Roho Mtakatifu nakuleta uhuru kwa
waliokandamizwa na dhambi na uovu. Yesu anaamsha tena matumaini yao katika ahadi za Mungu.
Yesu alikuja kutuweka huru kutoka katika dhuluma mbaya Zozote zile - katika utumwa wa dhambi. Injili ya kuongoka ni "habari njema" kwetu leo. Baada ya kuguswa na Yesu, ni zamu yetu kuwagusa wengine waweze kuhisi uwepo wa Yesu katika maisha yao.

Sala:
Bwana, sisi tunamkubali mwanao Yesu kama mkombozi wetu. Tunakuomba utusaidie kukomesha utumwa wetu katika dhambi.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni