Masomo ya Misa
Alhamisi baada ya Epifania (Alhamisi, Januari 09, 2020)
1Yoh 4:19-5:4
Wapenzi: Sisi twampenda Mungu kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende ndugu yake. Kila mtu aaminiye kwamba Yesu Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye. Katika hili twajua kwamba twapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo Imani yetu.
Zab 72:1-2, 14-15
Ee Mngu, mpe mfalme hukumu yako,
Na mwana wa mfalme haki yako.
Atawaamua watu wako kwa haki,
Na watu wako walioonewa kwa hukumu.
(K) Mataifa yote ya dunia watakusujudia, Ee Bwana.
Atawakomboa nafsi zao na kuonewa na udahlimu,
Na damu yao ina thamani machoni pake.
Na wamwombee daima;
Na kumbariki mchana kutwa.
(K) Mataifa yote ya dunia watakusujudia, Ee Bwana.
Jina lake na lidumu milele,
Pindi ling’aapo jua jina lake liwe na wazao;
Mataifa yote na wajibariki katika yeye,
Na kumwita heri.
(K) Mataifa yote ya dunia watakusujudia, Ee Bwana.
Lk 7:16
Aleluya, aleluya,
Nabii mkuu ametokea kwetu; na Mungu amewaangalia watu wake.
Aleluya.
Lk 4:14-22
Siku ile, Yesu alirudi kwa nguvu za Roho, akaenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando. Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote. Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ilia some. Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake.
Maoni
Ingia utoe maoni