Jumanne ya 10 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
1 Fal. 17:7-16Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako. Naye akasema, Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; name ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.
Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanya kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kasha ujifanyie nafsi yako na mwanao. Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi. Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya; nay eye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi.
Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa kinywa cha Eliya.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 4: 2-5, 7-8;Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo;
Umenifanyizia nafasi wakati wa shida;
Unifadhili na kuisikia sala yangu.
Enyi wanadamu,
Hata lini utukufu wangu utafedheheka?
K. Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Bali jueni ya kuwa Bwana amejiteulia mtauwa;
Bwana atasikia nimwitapo.
Mwe na hofu wala msitende dhambi,
Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
K. Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Wengi husema, Nani atakayetuonyesha mema?
Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Umenitia furaha moyoni mwangu,
Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.
K. Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Shangilio la Injili
Zab. 27:11Ee Bwana, unifundishe njia yako, na kuiongoza katika njia iliyonyoka.
Aleluya.
Injili
Mt 5: 13-16Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni