Jumanne, Juni 12, 2018
Jumanne, Juni 12, 2018,
Juma la 10 la Mwaka wa Kanisa
1 Fal 17: 7-16;
Zab 4: 2-5, 7-8;
Mt 5: 13-16
CHUMVI NA MWANGA
Yesu anawaambia Wafuasi wake: ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Ninyi ni mwanga wa ulimwengu. Maneno haya ni utangulizi wa maneno ambayo Yesu atayasema katika hutuba ya mlimani. Wafuasi wa Yesu wanatakiwa maneno ya Yesu yapenye ndani yao, yawatawale na wayaishi. Katika Agano la Kale, Waisrael walipewa amri kumi na Agano likafanywa kati yao likiwataka waishi kitakatifu na kwa haki kama wanavyotakiwa na Agano. Je, walitambua wao ni chumvi ya ulimwengu?. Walisisitiza sana kuhusu sheria, mpaka wakaua ile roho. Yesu anaonesha hili kwa wafuasi wake kwakuwaambia, wema wao usipozama ndani nakuushinda ule wa Walimu wa sheria na Mafarisayo, hawawezi kuwa chumvi ya ulimwengu. Yesu aliwataka Wafuasi wake wawe chumvi ya ulimwengu, si kwakusimama na kuonekana kama watakatifu bali kwa maadili mema na utu ambao umevishwa taji ya upendo kwa Mungu na kwa jirani. Kwa wema, maadili na utu huu uliovishwa taji, na kungarishwa na Imani, matumaini na mapendo, wakristo wanaalikwa kuwa mwanga wa Ulimwengu. Hawahitaji kujitangaza kwamba wao ni Wakristu. Wataonesha kwamba wao ni Wakristo “kwanjia hii wote watajua ya kuwa ninyi ni wafuasi wangu, kama mna pendana ninyi kwa ninyi” (Yn 13: 35).
Sala:
Bwana Yesu, nifanye mimi na watu walio karibu nami kuwa Wakristo wa kweli.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni