Alhamisi ya 21 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
1 The. 3: 7-13Basi Mungu mwenyewe, Baba yentu, na Bwana wetu Yesu, atuongoze na kuwazidisha katika upendo, ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu; apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 90:3-4, 12-14, 17Utushibishe kwa fadhili zako, tutashangili ana kufurahi.
Wamrudisha mtu mavumbini,
Usemapo, Rudini, enyi wanadamu.
Maana miaka elfu machoni pako
Ni kama siku ya jana ikiisha kupita,
Na kama kesha la usiku.
K. Utushibishe kwa fadhili zako, tutashangili ana kufurahi.
Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu,
Tujipatie moyo wa hekima.
Ee Bwana, urudi, hata lini?
Uwahurumie watumishi wako.
K. Utushibishe kwa fadhili zako, tutashangili ana kufurahi.
Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako,
Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.
Na uzuri wa Bwana, Mungu wetu, uwe juu yetu,
Na kazi ya mikono yetu utufanyie thabiti,
Naam, kazi ya mikono yetu uithibitishe.
K. Utushibishe kwa fadhili zako, tutashangili ana kufurahi.
Shangilio la Injili
Yn. 14: 5Bwana anasema:
Mimi ndimi njia, na ukweli, na uzima;
mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Aleluya.
Injili
Mt. 24: 42-51Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni