Jumamosi ya 18 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Hab 1:12-2:4Kwa sababu hiyo huutolea wavu wake sadaka na kulifukizia uvumba juya lake; kwa sababu kwa vitu vile fungu lake limenona, na chakula chake kimekuwa tele. Je! Atawatoa walio katika wavu wake, asiache kuwaua watu wa mataifa daima? Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu. Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia. Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa Imani yake.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 9:7–12Wewe Bwana, hukuwaacha wakutafutao.
Bwana atakaa milele,
Ameweka kiti chake tayari kwa hukumu.
Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki;
Atawaamua watu kwa adili.
K. Wewe Bwana, hukuwaacha wakutafutao.
Bwana atakuwa ngome kwake aliyeonewa,
Naam, ngome kwa nyakati ya shida.
Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe,
Maana Wewe, Bwana, hukuwaacha wakutafutao.
K. Wewe Bwana, hukuwaacha wakutafutao.
Mwimbieni Bwana akaaye Sayuni,
Yatangazeni kati ya watu matendo yake.
Maana mlipiza kisasi cha damu awakumbuka,
Hakukisahau kilio cha wanyonge.
K. Wewe Bwana, hukuwaacha wakutafutao.
Shangilio la Injili
Yn 10:27Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
Injili
Mt 17:14–20Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema, Mbona sisi hatukuweza kumtoa? Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa Imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na Imani kiasi cha punji ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowekana kwenu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
Jastune Akiza · 8 Agosti 2026
Hakika ukiamini bwana anatenda