Dominika ya 19 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
1Fal 19:9, 11-13Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 85:8-13Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako, Utupe wokovu wako.
Nisikie atakavyosema Mungu Bwana,
Maana atawambia watu wake amani.
Hakika wokovu wake u karibu na wamchao,
Utukufu ukae katika nchi yetu.
K. Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako, Utupe wokovu wako.
Fadhili na kweli zimekutana,
Haki na amani zimebusiana.
Kweli imechipuka katika nchi,
Haki imechungulia kutoka mbinguni.
K. Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako, Utupe wokovu wako.
Naam, Bwana atatoa kilicho chema,
Na nchi yetu itatoa mazao yake.
Haki itakwenda mbelc zake,
Nayo itazifanya hatua zake kuwa njia.
K. Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako, Utupe wokovu wako.
Somo la Pili
Rum 9:1-5kwamba nina huzuni nyingi na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu. Kwa maana ningeweza kuomba mimi mwenyewe niharimishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili; ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake; ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Lk 19:38Abarikiwe Mfalme ajaye kwa jina la Bwana;
Aleluya.
Injili
Mt 14:22-33Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (4)
Linus Bernard · 9 Agosti 2026
Wanaochapisha masomo ama Injili wafanye zoezi ya kuweza kurudia maandishi ili tunaposoma tuweze kupate raha kamili ya Bwana(kuna makosa madogo madogo katika maandishi). Amina
Kamgisha Elipidius · 9 Agosti 2026
Juma pili hii namshukuru mwenyezi mungu kwa kutuamsha salama .MAOMBI. Bwana nakuomba uniunganishe vema na familia yangu pia mjalie mke wangu asahau mawazo yote anayo yawazia mungu mlinde na mabaya yote anayoyawaza hakika ww ni ni mungu muweza wa yote nasema hayo kwa jina la mwanao yesu kristo amin...
Martin Mzopola · 9 Agosti 2026
Kweli wajitahidi kurudia moyo anaandika movo
Inocent Laurent · 9 Agosti 2026
Jumapili njema