Jumatatu ya 4 ya Mwaka
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Ebr. 11:32 – 40Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 31:19 – 23Iweni hodari, mpige moyo konde, nyinyi nyote mnamngojea Bwana.
Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako
Ulizowawekea wakuchao;
Ulizowatendea wakukimbiliao
Mbele ya wanadamu.
K. Iweni hodari, mpige moyo konde, nyinyi nyote mnamngojea Bwana.
Utawasitiri na fitina za watu
Katika sitara ya kuwapo kwako;
Utawaficha katika hema
Na mashindano ya ndimi.
K. Iweni hodari, mpige moyo konde, nyinyi nyote mnamngojea Bwana.
Bwana ahimidiwe;
Kwa maana amenitendea fadhili za ajabu
Katika mji wenye boma.
K. Iweni hodari, mpige moyo konde, nyinyi nyote mnamngojea Bwana.
Nami nalisema kwa haraka yangu,
Nimekatiliwa mbali na macho yako;
Lakini ulisikia sauti ya dua yangu wakti nilipokulilia.
K. Iweni hodari, mpige moyo konde, nyinyi nyote mnamngojea Bwana.
Mpendeni Bwana, ninyi nyote mlio watauwa wake.
Bwana huwahifadhi waaminifu,
Humlipa atendaye kiburi malipo tele.
K. Iweni hodari, mpige moyo konde, nyinyi nyote mnamngojea Bwana.
Shangilio la Injili
Yn. 15:15Bwana anasema: Siwaiti tena watumwa, lakini ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.
Aleluya.
Injili
Mk. 5:1 – 20Na laipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia; akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi. Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile. Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha. Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao. Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini.
Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashamba. Watu wakatoka walione lililotokea. Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, ndiye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa. Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe. Wakaanza kumsihi aondoke mipakani mwao.
Naye alipokuwa akipanda chomboni, yule aliyekuwa na pepo akamsihi kwamba awe pamoja naye; lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu. Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni