Jumatano. 30 Oktoba. 2024

Masomo ya Misa

Jumatano ya 4 ya Mwaka (Jumatano, Februari 01, 2017)  

Somo la 1

Ebr. 12;4 – 7, 11 – 15

Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi. Tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, wala usizimie moyo ukikemewa naye; maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, naye humpiga kil amwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimi; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi aisyerudiwa na babaye? Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye Amani. Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kipnywe. Tafuteni kwa bidii kuwa na Amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; mkiangalia kana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.

Wimbo wa Katikati

Zab. 103:1 – 2, 13 – 14, 17 – 18

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana
Naam, vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi jina lake takatifu.
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,
Wala usizisahau fadhili zake zote.
(K) Fadhili za Bwana zina wamchao tangu milele hata milele


Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake,
Ndivyo Bwana awahurumia wamchao.
Kwa maana yeye anatujua umbo letu
Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.
(K) Fadhili za Bwana zina wamchao tangu milele hata milele


Fadhili za Bwana zina wamchao
Tangu milele na milele,
Na haki yake ina wana wa wana;
Wale washikao agano lake.
(K) Fadhili za Bwana zina wamchao tangu milele hata milele

Shangilio

Yn. 8:12

Aleluya, aleluya,
Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana, yeye anifuataye hatakwenda gizani na kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.

Injili

Mk. 6:1-6

Yesu alitoka huko, akafika mpaka nchi ya kwao, wanafunzi wake wakamfuata. Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jaama zake, na nyumbani mwake. Wala hakuweza kufanya mwujiza wowote huko; isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya. Akastaajabu kwa sababu ya kutokuamini kwao.

Maoni


Ingia utoe maoni