KUMBUKUMBU YA MT. FARANSISKO WA SALES (ASKOFU NA M
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Ebr. 10:1 – 10Dhabihu na toleo hukutaka, lakini mwili uliwekea tayari; sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) niyafanye mapenzi yako, Mungu.
Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendwazwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati), ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 40:1, 3, 6 – 7, 10Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja, kuyafanya mapenzi yako.
Nalimngoja Bwana kwa saburi,
Akaniinamia akakisikia kilio changu.
Akatia wimbo mpya kinywani mwangu
Ndio sifa zake Mungu wetu.
K. Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja, kuyafanya mapenzi yako.
Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo,
Masikio yangu umeyazibua,
Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.
Ndipo niliposema, Tazama nimekuja.
K. Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja, kuyafanya mapenzi yako.
Nimehubiri habari za haki
Katika kusanyiko kubwa,
Sikuizuia midomo yangu;
Ee Bwana, unajua.
K. Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja, kuyafanya mapenzi yako.
Sikusitiri haki yako moyoni mwangu,
Nimetangaza uaminifu wako na wokovu wako.
Sikuficha fadhili zako wala kweli yako
Katika kusanyiko kubwa.
K. Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja, kuyafanya mapenzi yako.
Shangilio la Injili
Yak. 1:21Pokeeni kwa upole neno la Mungu lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
Aleluya.
Injili
Lk. 10:1-9Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni