Ijumaa ya 1 ya Mwaka
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Ebr. 4:1 – 5, 11Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu yeyote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 78:3 – 4, 6 – 8Msiyasahau matendo ya Mungu.
Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu,
Ambayo baba zetu walituambia,
Tukiwaambia kizazi kindine
Sifa za Bwana na nguvu zake.
K. Msiyasahau matendo ya Mungu.
Wasimame na kuwaambia wana wao,
Wamwekee Mungu tumaini lao,
Wala wasiyasahau matendo ya Mungu,
Bali wazishike amri zake.
K. Msiyasahau matendo ya Mungu.
Wasiwe kama baba zao,
Kizazi cha ukaidi na uasi,
Kizazi kisichojitengeneza moyo,
Wala roho yake haikuwa amini kwa Mungu.
K. Msiyasahau matendo ya Mungu.
Shangilio la Injili
Yn. 17:17Neno lako ndiyo kweli, Ee Bwana, ututakase kwa ile kweli.
Aleluya.
Injili
Mk. 2:1-12Naye Yesu, alipoiona Imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako. Na baadhi yay a waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao, Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?
Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende? Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza), Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende nyumbani kwako. Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni