Jumapili. 24 Novemba. 2024

Masomo ya Misa

Jumanne ya 1 ya Mwaka (Jumatano, Januari 11, 2017)  

Somo la 1

Ebr. 2:14 – 18

Kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeyey naye vivyo hivyo alishiriki yay ohayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, ayani, Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.; maana ni hakika, hatwai asili ya malika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.

Wimbo wa Katikati

Zab. 105:1 – 4, 6 – 9

Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake,
Wajulisheni watu matendo yake.
Mwimbieni kwa zaburi,
Zitafakarini ajabu zake zote.
(K) Bwana analikumbuka agano lake milele.


Jisifuni kwa jina lake takatifu,
Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana,
Mtakeni Bwana na nguvu zake,
Utafuteni uso wake siku zote.
(K) Bwana analikumbuka agano lake milele.


Enyi wana wa Ibrahimu, mtumishi wake;
Enyi wana wa Yakobo wateule wake.
Yeye Bwana, ndiye Mungu wetu;
Duniani mwote mna hukumu zake.
(K) Bwana analikumbuka agano lake milele.


Analikumbuka agano lake milele,
Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
Agano alilofanya na Ibrahimu,
Na uapo wake kwa Isaka.
(K) Bwana analikumbuka agano lake milele.

Shangilio

Efe. 1:17, 18

Aleluya, aleluya,
Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, awape roho ya hekima mjue tumaini la mwito wake.
Aleluya.

Injili

Mk. 1:29-39

Siku ile, Yesu alipotoka katika sinagogi, walifika nyumbani kwa Simoni na Andrea, pamoja na Yakobo na Yohane. Naye mkewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani, hawezi homa; na mara wakamwambia habari zake. Akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha, akawatumikia. Hata kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, walikuwa wakimletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo. Na mji wote ulikuwa umekusanyika mlangoni. Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua. Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko. Simoni na wenziwe wakamfuata; nao walipomwona wakamwambia, Watu wote wanakutafuta. Akawaambia, Twendeni mahali pengine, mpaka vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nako; maana kwa hiyo nalitokea. Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo.

Maoni


Ingia utoe maoni