Ijumaa. 22 Novemba. 2024

Masomo ya Misa

Jumamosi ya 7 ya mwaka (Jumamosi, Mei 25, 2024)  

Somo la 1

Yak 5:13–20

Mtu wa kwenu amepatika na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi. Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na waite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa Imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa. Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpatate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi akaomba kwa bidii mvua isinye; na mvua haikunya juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake. Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza; jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.

Wimbo wa Katikati

Zab 141: 1–3, 8

Ee Bwana, nimekuita, unijie hima,
Uisikie sauti yangu nikuitapo.
Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba,
Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.
(K) Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba.

Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu,
Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.
Macho yangu yanakuelekea Wewe, Mungu Bwana,
Nimekukimbilia Wewe, usiniache nafsi yangu.
(K) Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba.

Shangilio

Yn 17:17

Aleluya, aleluya.
Neno lako ndiyo kweli, ee Bwana, ututakase kwa ile kweli.
Aleluya.

Injili

Mk 10:13–16

Makutano walimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea. Ila Yesu alipoona alichukuzwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni, Yeyote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa. Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki.

Maoni

Martin Muteti

Amina

Ingia utoe maoni