Ijumaa ya 9 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Tob. 11:5-15Rafaeli akamwambia Tobia, Najua ya kuwa baba yako atafumbua macho yake. Basi umtie mara nyongo machoni; na imchomapo atajifikicha; na vyamba vyeupe vitaambuka; atakuona kwa macho.
Lakini Ana alimkimbilia, akamwangukia mwanawe shingoni, akamwambia, Mwanangu! Nimekuona; tangu sasa ni radhi nife. Wakalia wote wawili. Tobiti naye akaondoka kwenda mlangoni, akajikwaa; lakini mwanawe akamkimbilia, akamshika baba yake; akamtia nyongo machoni, akasema, Jipe moyo, baba yangu. Yeye macho yake yalipoanza kuwasha aliyefikicha; navyo vyamba vyeupe vikaambuka katika pembe za macho yake, akamwona mwanawe, akamwangukia shingoni. Akalia, akasema, Ee Mungu umehimidiwa; na jina lako limehimidiwa milele; na watukuzwe malaika zako watakatifu wote. Kwa maana umenirudi, ukanihurumia; lo-o—o; namwona mwanangu Tobia.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 145:1,7-10Ee nafsi yangu, umsifu Bwana.
Aleluya.
Ee nafsi yangu, umsifu Bwana.
Nitamsifu Bwana muda ninaoishi,
Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.
K. Ee nafsi yangu, umsifu Bwana.
Au: Aleluya.
Huishika kweli milele,
Huwafanyia hukumu walioonewa.
Huwapa wenye njaa chakula;
Bwana hufungua waliofungwa.
K. Ee nafsi yangu, umsifu Bwana.
Au: Aleluya.
Bwana huwafumbua macho waliopofuka;
Bwana huwainua walioinama;
Bwana huwapenda wenye haki;
Bwana huwahifadhi wageni;
Huwategemeza yatima na mjane.
K. Ee nafsi yangu, umsifu Bwana.
Au: Aleluya.
Bwana atamiliki milele,
Mungu wako, ee Sayuni,
Kizazi hata kizazi.
K. Ee nafsi yangu, umsifu Bwana.
Au: Aleluya.
Shangilio la Injili
Zab. 111 :7, 8Unitie nguvu sawasawa na neno lako, ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Aleluya.
Injili
Mk. 12:35-37Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni