Dominika ya 27 ya Mwaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Hab. 1:2 – 3; 2:2 – 4Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 95:1 – 2, 6 – 9Ingekuwa heri leo tusikie sauti yake! Tusifanye migumu mioyo yetu.
Njoni tumwimbie Bwana,
Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.
Tuje mbele yake kwa shukrani,
Tumfanyie shangwe kwa zaburi.
K. Ingekuwa heri leo tusikie sauti yake! Tusifanye migumu mioyo yetu.
Njoni, tuabudu tusujudu,
Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba.
Kwa maana ndiye Mungu wetu,
Na sisi, tu watu wa malisho yake,
Na kondoo za mkono wake.
K. Ingekuwa heri leo tusikie sauti yake! Tusifanye migumu mioyo yetu.
Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!
Msifanye migumu mioyo yenu;
Kama huko Meriba;
Kama siku ile ya Musa jangwani,
Hapo waliponijaribu baba zenu,
Wakanipima, wakayaona matendo yangu.
K. Ingekuwa heri leo tusikie sauti yake! Tusifanye migumu mioyo yetu.
Somo la Pili
2Tim. 1:6 – 8; 13 – 14Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Yn. 15:15Ninyi nimewaita rafika,
kwa kuwa yote niliyoyasikia
kwa baba yangu nimewaarifuni.
Aleluya!
Injili
Lk. 17:5 – 10Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng’ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula? Je! Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa? Je! Atampa asante yule mtumwa; kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa? Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni