Jumapili, Oktoba 02, 2016
Jumapili, Oktoba 2, 2016.
Dominika ya 27 ya Mwaka
Hab 1:2-3; 2:2-4
Zab 95: 1-2, 6-9
2 Tim 1: 6-8, 13-14
Lk 17: 5-10
KUSALI KWA IMANI!
Biblia haijasema kama Abrahamu alienda kwenye mapango kusali lakini anachukuliwa Baba wa imani: baba wa imani na mfano wa sala. Maisha Yake yanatawaliwa na sala na imani; alifanya vitu tu baada ya kusikia sauti ya Mungu; alichukua jukumu na kutekeleza na kushika njia mara baada ya kusikia neno la Bwana. Maisha Yake yanatawaliwa na mazungumzo baina Yake na Mungu. Mungu alimwambia Abram: nenda....Abram akaondoka... (Mwa 12:1,4)... " Neno la Mungu lilimjia Abram katika ndoto ..... na Abram akasema: Bwana utanipa nini Mimi?”… (Mwa 15:1,2). Bwana alimtokea katika Mamre na hapo akainamisha kichwa chake ardhini" Mwa 18:1-3). “Bwana alimjaribu Abram... Abram akajibu nipo hapa!”(Mwa 22:1) mazungumzo haya yaliijaza imani ya Abraham, yalimwandaa kupokea mapenzi ya Mungu.
Nabii Habakuki aliishi na changamato nyingi sana katika imani Yake. Ukosefu wa Haki, maovu katika jamii yanaonesha Mungu hapendezwi na haingilii kati. Habakkuki ana jaribu Kuelewa yanayotea na haogopi kuanza masungumzo na Mungu. Anathubutu kumuuliza Mungu kwa ujasiri kwamba anapingana naye, kwamba haelewi kukaa kwake kimya bila kutenda kitu dhidi ya maovu, anamkumbusha juu ya ukimya wake na kutokufanya kitu; anathubutu kumwambia atoe hesabu ya njia zake juu ya kuutawala ulimwengu na matukio ya kihistoria. Baada ya kutoa malalamiko yake, na juu ya uovu wa watu, nabii anakaa kimya. Ni wakati wa Mungu kujibu. Mungu anajibu, hatoi maelezo yeyote, anadai juu ya uaminifu usio na masharti. Anajua juu ya mapungufu ya nabii na ya watu; alijua kwamba hawawezi kuelewa sababu ya ukimya wake wakutokufanya kitu. Badala yake anatoa uhakika kwamba kilichosemwa leo siku moja kitaeleweka kwa wote.
Katika somo la pili mtume Paulo pia anaongelea kuhusu imani. Timoteo anaongelea kuhusu kuwa na imani, kwa njia yake kueneza matendo ya huruma. Mfuasi pia anaalikwa kuwa mkarimu katika Imani, zawadi ya Mungu ambayo ipo ndani yake na kwanjia ya kuwekea mikono, anasimikwa kama zawadi, aliyopokea ili aweze kuchukua kazi zake za kitume kama msaidizi wa Paulo. (2 Tim 1: 6).
“Imani” katika uhalisia ni kujikita kwa mtu, kujikabidhi kwa mtu, uaminifu, na mshikamono unaotoka katika uaminifu huo. Ndio kusema, mitume hawamuombi Yesu kuongeza uelewa wao au akili zao kuhusu mambo. Wanamuomba Yesu aongeze uaminifu wao kwake. Yesu bila kujibu moja kwa moja sala yao, anatumia njia nyingine na anatumia taswira ya picha kuelezea hali ya juu ya Imani na umuhimu wake. Kama vile Kamba yaweza kushikilia kitu kizito kuliko kamba yenyewe, ndivyo ilivyo kwa Imani kidogo, inaweza kufanya kitu kikubwa ambacho huwezi kufikiria, kitu cha hali ya juu, kama vile kungoa mti mkubwa na kuupanda baharini. Imani, ndio kusema, kumuamini Kristo, kumkaribisha, na kumfanya atubadilishe, kumfuata mpaka mwisho kabisa, inafanya mambo ya mwanadamu yasiowezekana yawezekane katika hali zote.
Mbegu ni kwa ajli ya kupanda, ili vitu vingine vizuri zaidi vinavyopendwa viote. Tunapo otesha mbegu ya Imani yetu, inasababisha Imani zaidi iweze kukuwa, na matendo ya Imani, ambayo ni upendo wa Mungu, haki na huruma. Kwa njia hii tunaleta upendo wa Mungu kwa wasio pendwa, nakupenda, huruma ya Mungu kwa wasio na huruma na kwa wote ambao hawajaitambua huruma ya Mungu maishani mwao. Tunafanya haki ya Mungu ikuwe katika maeneo yasio na upendo, yenye vita na dhuluma, na kwa mioyo isio na haki. Tuna sababisha Imani ikuwe kwenye mioyo ya watu ambao hawakuwa na Imani, au kwa walio poteza Imani yao kwasababu ya kuboreka na kupoteza tumaini. Kwa kupanda na kupalilia mbegu ya Imani, tunakuta na Imani yetu wenyewe inakuwa, na jukumu kama kusamehe, kila mara inamfanya mtu iwe rahisi na neema kukuwa zaidi, ni kama sehemu za kazi katika maisha yetu, kadiri tufanyavyo kazi flani ndivyo inakuwa rahisi na nyepesi katika kuitenda: mfano pia, kucheza mpira, kucheza ala za muziki, kutengeneza picha nk. Imani yetu inatosha na ni muhimu. Tuna sehemu ya kusimamia na kuwa vyote anavyotaka Mungu.
Matukio mengi katika maisha yetu yanaweza kuonekana ya kushangaza na hayafikiriki na yanatufanya tuwe na maswali kuhusu uwepo wa Mungu. Kipindi hiki Imani yetu inawekwa kwenye majaribu makubwa, na mara nyingi tunamlilia Mungu na kumuomba msaada. “Bwana sikia sala yangu” sikiliza kilio chetu”. Mungu kila wakati anasikia sauti zetu ingawaje ni vigumu kwetu kutambua sauti yake. Sala ndio inayo fungua moyo wetu, inatusaidia kuelezea mahitaji yetu, ulinzi wetu na mipango yetu na hapo kutufanya sisi tuyakaribishe mapenzi ya Mungu katika maisha yetu. Tutafute Imani iliojitosheleza na thabiti kwa Mungu kwa njia ya sala. Imani tukiwa katika mateso yetu, Imani kuona mapenzi ya Mungu yametimia katika maisha yetu.
Sala: Bwana Yesu, ongeza Imani yetu na utufanye tuwe watumishi wako wa aminifu, ili tuendelee kufanya utume wako na kukushuhudia Wewe. Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni