Jumanne. 26 Novemba. 2024

Masomo ya Misa

Jumanne ya 16 ya Mwaka (Jumanne, Julai 20, 2021)  

Somo la 1

Kut 14:21-15:1

Musa alinyosha mkono wake juu ya bahari; Bwana akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika Wana wa Israeli wakaenda ndani kati ya bahari katika nchi kavu; nayo maji yalikuwa ukuta kwao mono wa kuume, na mkono wa kushoto. Na wale Wamisri wakawafuatia, wakaingia ndani kati ya bahari, farasi zote za Farao, na magari yake, na wapanda farasi wake. Ikawa katika zamu ya alfajiri, Bwana akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha jeshi la Wamisri. Akayaondoa magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa uzito; na Wamisri wakasema, Na tukimbie mbele ya Israeli; kwa kuwa Bwana anawapigania, kinyume cha Wamisri. Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao. Musa akaunyosha mkoon wake juu ya bahari, na kulippambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na Bwana akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari. Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja. Lakini wana wa Israeli wakaenda katika nchi kavu katikati ya bahari; na hayo maji yalikuwa ni makuta upande wao wa kuume, na upande wao wa kushoto. Ndivyo Bwana alivyowaokoa Israeli siku ile mikononi mwa Wamisri; Waisraeli wakawaona Wamisri ufuoni kwa bahari, wamekufa. Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya Bwana juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha Bwana, wakamwamini Bwana, na Musa mtumishi wake. Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia Bwana wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.

Wimbo wa Katikati

Zab 15:8-10, 12, 17

Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa,
Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu,
Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.
Adui akasema Nitafuatia, nitapata nitagawanya nyara,
Nafsi yangu itashibishwa na wao;
Nitaufuta upanga wangu,
Mkono wangu utawaangamiza.
(K) Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana.

Ulinyosha mkono wako wa kuume,
Nchi ikawameza.
Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza;
Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu.
(K) Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana.

Utawaingiza, na kuwapanda
Katika mlima wa urithi wako,
Mahali pale ulipojifanyia, Ee Bwana, ili upakae,
Pale patakatifu ulipopaweka imara, Bwana,
Kwa mikono yako.
(K) Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana.

Shangilio

Zab 130:5

Aleluya, aleluya,
Roho yangu inamngoja Bwana, na neno lake nimelitumainia.
Aleluya.

Injili

Mt 12:46–50

Yesu alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje wataka kusema naye. Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe. Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani? Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu! Kwa maana yeyote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.

Maoni


Ingia utoe maoni