Kumbukumbu ya Mt. Alfonsi Maria Liguor
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer 26:11–16, 24Ndipo wakuu na watu wote wakawaambia makuhani, na manabii, wakisema, Mtu huyu hastahili kuuawa; kwa maana amesema nasi katika jina la Bwana, mungu wetu. Mkono wa Ahikamu, mwana wa Shafani, ulikuwa pamoja na Yeremia, wasimtie katika mikono ya watu auawe.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 69:14–15, 29–30, 32–33Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Ee Mungu.
Uniponye kwa kunitoa matopeni,
Wala usiniache nikazama.
Na niponywe nao wanaonichukia,
Na katika vilindi vya maji.
Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze,
Wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu.
K. Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Ee Mungu.
Nami niliye maskini na mtu wa huzuni.
Mungu, wokovu wako utaniinua.
Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,
Nami nitamtukuza kwa shukrani.
K. Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Ee Mungu.
Walioonewa watakapoona watafurahi,
Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.
Kwa kuwa Bwana huwasikia wahitaji,
Wala hawadharau wafunga wake.
K. Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Ee Mungu.
Shangilio la Injili
Zab 119:18Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako.
Aleluya.
Injili
Mt 14:1–12Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni