Jumanne. 26 Novemba. 2024

Masomo ya Misa

Jumatatu ya 31 ya Mwaka (Jumatatu, Novemba 05, 2018)  

Somo la 1

Flp. 2:1 – 4

Ikiwako faraja yoyote katika Kristo, yakiwako matulizo yoyote ya mapenzi, ukiwako ushirika wowote wa Roho, ikiwako huruma yoyoe na rehema, ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja. Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.

Wimbo wa Katikati

Zab. 131

Bwana, moyo wangu hauna kiburi,
Wala macho yangu hayainuki.
Wala sijushughulishi na mambo makuu,
Wala na mambo yashindayo nguvu zangu.
(K) Moyo wangu uwe na amani kwako, Ee Bwana.

Hakika nimeituliza nafsi yangu,
Na kuinyamazisha.
Kama mtoto aliyeachishwa
Kifuani mwam mama yake;
Ndivyo roho yangu ilivyo kwangu.
(K) Moyo wangu uwe na amani kwako, Ee Bwana.

Ee Israeli, umtarajie Bwana,
Tangu leo na hata milele.
(K) Moyo wangu uwe na amani kwako, Ee Bwana.

Shangilio

Zab. 130:5

Aleluya, aleluya,
Roho yangu inamngoja Bwana, na neno lake nimelitumainia.
Aleluya.

Injili

Lk. 14:12 – 14

Yesu alimwambia yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu, nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.

Maoni


Ingia utoe maoni