Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Januari 06, 2019

Januari 6, 2019.

------------------------------------------------

JUMAPILI, SHEREHE YA EPIFANIA (TOKEO LA BWANA)

Somo la 1: Isa 60:1-6 Nabii Isaya anatoa utabiri wa Yerusalemu yenye furaha na kurudi kutoka kwao utumwani, lakini maono haya yalikuwa yakitabiri ujio wa Kristo ambaye ataunganisha mataifa yote.

Wimbo wa katikati Zab 72:1-2, 7-8, 10-13 Mataifa yote ya ulimwengu yatakuja kukusujudu wewe Bwana. Mbele yako wafalme wote watasujudu na kukutumikia.

Somo 2: Efe 3:2-3, 5-6 Paulo anatoa siri ya utume wake: ametumwa na Mungu kuja kuhubiri habari njema kwa watu wa mataifa yote, watu ambao Mungu amewachaguwa kuwa wake pamoja na Wayahudi.

Injili: Mt 2:1-12 Tunaona Mamajusi watatu wakienda Betlehemu na kumchukulia mtoto Yesu zawadi na kumwabud.
.
------------------------------------------------

KILA GOTI LITAPIGWA KWAKE ( Fil 2:10)!

Katika somo la kwanza, katika ono lake la kinabii, Isaya
anaona ujio wa Mungu ulimwenguni. Utakuja muda ambapo
watu wote wataletwa pamoja mbele ya Bwana na
watabarikiwa sana. Utukufu wa Bwana utashuka
ulimwenguni na utukufu wake utauzunguka uumbaji wote.
Tukio hili takatifu litalibadilisha jiji la Yerusalemu na wale
wote wanaofanya kazi na kuvumilia watapokea mwanga wa
uhai.

Katika somo la pili, Paulo anaifumbua siri ambayo Mungu
anaitoa kwa utukufu wake watu wote pamoja na wapagani,
kuwafanya warithi wa ufalme wake. Anasema “sasa
imefunguliwa kuwa wapagani wanashiriki urithi ule ule”.
Ukombozi wa ulimwengu, Mungu pia anawapenda wasio
Wakristo kwani wao pia ni wapokeaji.

Leo tunasherehekea sherehe ya Tokeo la Bwana. Ni sherehe
ya dhihirisho la Bwana wetu kwa watu wa Mataifa.
Kulikuwa na mama jusi watatu kutoka mashariki waliokuja
kwa Mfalme mpya aliyezaliwa. Mama jusi hawa, watu wa
mataifa, ambao hawakuwa katika utajiri wa pamoja wa
Waisraeli, walikuwa ni watu waliosoma nyota kwa lengo la
kubaini siri na ujumbe wake. Walipokuja katika mahakama
ya mfalme, walimuuliza Herode, yuko wapi mfalme wa
Wayahudi aliyezaliwa? Hawakuuliza kama mfalme wa
wayahudi amezaliwa? Walikuwa na uhakika kuwa mfalme
alikuwa amekwisha zaliwa. Walikuwa tu hawana uhakika wa
sehemu yake alipozaliwa, bali juu ya ukweli kwamba amezaliwa walikuwa nao.

Kama tu vile Yeye alivyo jidhihirisha Yeye Mwenyewe kwa wale mama
jusi, kila siku Mungu anajidhihirisha mwenyewe kwetu sisi
katika Ekaristi Takatifu. Tunamtukuza Yeye, tunamshukuru
na kumfanya yeye afahamike ulimwenguni kote. Basi tujitoe
sisi wenyewe kama zawadi na tuunganike naye na kuhubiri:
Mungu amejidhihirisha mwenyewe duniani. Yesu anajitoa
mwenyewe zawadi kwa dunia nzima.


Sala:
Bwana, niwezeshe niweze kujitoa Mimi mwenyewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni