Imani Iliyo Jaribiwa
· na Shajara Administrator
Nguvu na uwezo unajaribiwa zaidi ya kuwa na vyeti. Hii ni kweli pia katika Imani yetu. Sio wengi watakao simama katika kujaribiwa huku kwa Imani. Yesu analifahamu hili na anataka kutoa somo kamili katika Injili. Masharti yake kama vile, ‘Kama” “Lakini” yanamuonesha wito wake kwetu wa kuwa makini. Haongei kwa mafumbo wala mfano. Anataka Imani kamili isiotikiswa kwa Mungu na msukumo kamili katika kumfuata Yeye katika hali zote.
Kukubali kwamba wewe ni Mkristo kwa baadhi ya Nchi inamaana umejitangazia kifo. Na sehemu nyingine, ina maana umejitangazia, mateso, kukataliwa baadhi ya huduma au kuto kuchaguliwa kwa ajili ya jambo flani. Ni katika hali hiyo pia kumkubali Kristo inaweza kuhatarisha mambo binafsi, usalama wako wa kifedha na umuhimu wako pengine. Lakini Yesu anasisitisa kwamba kama tunataka kukubaliwa mbinguni mbele ya Malaika watakatifu kama watoto wa kweli wa Mungu, tunapaswa kukiri ukweli huo mbele ya ulimwengu, hata katika mateso na kutengwa.
Sala:
“Kusiwe na kitu cha kukusumbua. Kila kitu kitapita. Mungu habadiliki. Uvumilivu unapata mambo yote. Hahitaji kitu mtu aliye na Mungu. Mungu mwenyewe anatenda”.
Amina.

Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni