Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Septemba 30, 2018

Jumapili, Septemba 30, 2018.
Dominika ya 26 ya Mwaka B wa Kanisa

Hek 11; 25-29;
Zab 18: 8, 10, 12-14;
Yak 5 1-6;
Mk 9: 38-43, 45, 47-48.


JE, WEWE NI JIWE LA KUZUIA WENGINE AU JIWE LA KUVUSHIA WENGINE?


Ulimwengu umekuwa mdogo sana. Watu wanaishi karibu zaidi kuliko zamani. Wanahitajiana kila siku hata zaidi ya zamani. Kwahiyo kila mmoja anahitajika kwa hali kubwa. Mkristo anapaswa kutambua kwamba namna anavyoishi inagusa maisha ya mwingine labda kwa uzuri kama anaishi vizuri au kwa ubaya kama anaishi vibaya. Nipende nisipende naweza kuwa jiwe la kuzuia kwa ndugu zangu au jiwe la kuwavusha wengine katika barabara ya wokovu. Hili ni muhimu kwa watu wa aina zote: wadogo, wakubwa, wenye ndoa, wazazi, walioajiriwa nk.

Mmoja anaweza kuwa jiwe la kuzuia namna gani?:

1. Wakati tunapokuwa sio wakarimu na wasio haki tunapowatenda wengine. Unawafanya wadogo na kuharibu utu wao na kuharibu ujasiri wao.

2. Tunapo shindwa kuelewa mapungufu ya wengine, maanguko yao, dhambi zao na kuwatupilia mbali. Tunapo wahukumu wengine tunawafanya wajisikie wao ni waovu mnoo.


3. Tunapo wahukumu wengine kwasababu hawaishi kama tunavyopenda. Tunawaumiza na kuharibu taswira yao.

4. Tunapo wakatisha tamaa wengine, kuwaweka chini na kuwafanya wasiinuke. Pale tunapozuia mwanga wao na kujikuta wakitembea katika giza na kujihisi wanyonge.


5. Wakati unapowakataa wengine, tunapo watenga na kuwakataa. Tunawafanya wajisikie wao ni waliokataliwa na wasiofaa.

6. Wakati tunapowakosoa wengine kwa upinzani mkali bila kuwa na mapendo. Tunararua kabisa mawazo yao na sisi kuwa kovu katika matumaini yao.


7. Tunapo wanyonya wengine kwakuwalipa mshahara kidogo. Tunawafanya wawe kama watumwa na sisi kuishi kama Mabwana. Tunawakandamiza ili sisi tubaki na nguvu.


Tukifanya kati ya haya kwa wengine, sisi tunakuwa giza kwao, sisi ni kuzuizi katika njia zao. Sisi ni vizuizi katika njia za wengine, na tunawafanya waone ugumu katika kuufikia Ufalme wa Mbinguni. Hili ni nila muhimu kweli.

Lakini, pia tunaweza kuwa Jiwe la kuvushia wengine.

1. Wakati tunapo wasaidia wengine wakati wa madhaifu na wasiwasi.

2. Tunapowapa Imani wengine, wakati tunapo inua ujasiri wao na tunapo ona kitu ndani yao ambacho wao wenyewe wanashindwa kuona.


3. Wakati wanapojisikia hawajiwezi na kuwasaidia ili waweze kutambua vipaji vyao alivyowapatia Mungu.

4. Tunapo wapa changamoto, bila kuwaumiza na kuwasaidia kukuwa katika mawazo yao.

5. Tunapokataa kujiunga na makundi ili kuwarushia mawe au lawama kwasababu ya dhambi yao.


6. Tunapo wasamehe. Tunawanasua kutoka katika mambo yao ya zamani na kuwafanya wasonge mbele.

7. Wakati tunapo waelewa na kuwasikiliza na wao kujisikia kama sisi ni dada na kaka zao.


8. Wakati tunapo kataa kuwanyanyasa au kujichukulia umaarufu kwasababu ya mapungufu yao.


Kama tumefanya kati ya haya kwao, sisi tumekuwa mwanga kwao katika giza lao. Sisi tunakuwa kama kibao cha kuelekeza wakati wakiwa katika matatizo namashaka. Sisi tunakuwa kivuko katika mawimbi mengi ya dhoruba za maisha. Sisi tunakuwa mfano kwao na rafiki wa kweli.

Yesu anasema kwamba kama mmoja akimpatia kikombe kidogo cha maji ya baridi atarudishiwa daima. Tunapaswa kufanya hivyo kwa kuwaelekeza wengine katika kisima chetu na kuwashirikisha maji yako.
Tafakari leo juu ya mahusiano yako. Kama una rafiki wa karibu katika maisha yako tafakari jinsi unavyo msaidia huyo mtu au ni kwa jinsi gani anakusaidia. Hakikisha Yesu yupo katikati daima katika mahusiano haya na kiini chenu.


Sala:
Baba wa Mbinguni, sisi ni wadhaifu daima tuliotiwa sumu na dhambi. Tunaomba neema ili tusiweze kuangushwa chini wala kuwaangusha wenzetu kwenye dhambi. Saidia mikono hii uiongoze katika njia ya uzima wa milele. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni