Jumanne, Julai 17, 2018
Jumanne, Julai 17, 2018,
Juma la 15 la Mwaka
SOMO 1
Isa. 7: 1 – 9
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 48: 1 – 7 (K) 8
Mt 11:20-24
AMKA NA UITIKE WITO!
Katika somo la Injili Yesu anaongea na watu wa mji ambao amefanya miujiza mingi na uponyaji, lakini watu wanaendelea na mambo yao ya kawaida kama vile hakuna kitu kinacho tokea kati yao. Yesu anawaambia waamke na kutubu! Wanachagua wenyewe kuteseka milele na maangamizi. Sidhani kama kuna mmoja wetu anaweza kutamani kuchagua jambo kama hilo kuteseka milele au mtu mwingine ateseke milele. Yesu yupo hapa, yupo nasi leo, tunapaswa kujikita katika ukweli huu. Tunapaswa kumgeukia yeye, na kumwambia utusamehe kwa yale yote ambayo tumekutendea, na hivyo kukabidhi maisha yetu kwake.
Yesu anawakemea watu wa Korazini na Betsaida kwasababu anawapenda anaona wanabaki tu katika maisha yao ya dhambi ingawaje ameleta habari njema na miujiza mingi mikubwa. Walibaki katika hali ya usumbufu, mtegoni, kuchanganyikiwa, kukataa kutubu, na hali ya kutokuwa tayari kubadilisha njia zao za maisha. Yesu anaonesha hali ya huruma ya hali ya juu. Yesu anawaonya. Yesu anawaonya katika hali ya upendo na kutaka wabadilike. Hawakubadillika mara moja baada ya yeye kuwaalika kwa kufanya miujiza mingi, hivyo alipenda kubadilisha hali na kuleta hali mpya. Tafakari leo, kama unataka Yesu akuongoze kwa mapendo utoke katika hali yako , kama unapenda kukubali Injili ya upendo izame ndani yako.
Sala:
Bwana, nisaidie mimi niweze kuungama dhambi zangu daima. Nisaidie niweze kuwa chombo cha kuwafanya wenzagu wakurudie. Ninaomba nipokee siku zote neno lako kwa upendo na kulishirikisha kwa upendo katika hali inayo faa. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni