Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Disemba 30, 2017

Desemba 30, 2017. 

------------------------------------------------

JUMAMOSI, OKTAVA YA NOELI


Somo la 1: 1 Yn 2:12-17 Yohane anaendelea kutuhubiria sisi tena na kutukumbusha juu ya jukumu letu kama Wakristo, na hasa juu ya sisi kuwa macho kwasababu ya malimwengu. 


Wimbo wa Katikati Zab: Ps 95: 7-10 Mbingu na zifurahi nchi na ishangilie. Mwabuduni Bwana hekaluni mwake. Ee Dunia tetemeka mbele za Bwana.


Injili: Lk 2: 36-40 Anna, nabii mwanamke, anasali kwa ujasiri kama Simeoni kwa ajili ya Mkombozi. Wakati alipo muona, na kumpa Mungu shukrani na anaondoka na kwenda kumwambia kila mmoja kuhusu hili. 

------------------------------------------------


JIBU LA KUKUMBANA NA KIPINDI CHETU CHA NOELI 

Leo katika siku ya sita ya oktava ya Noeli, tunamheshimu nabii Anna. Jana Semoni aliye oneshwa kama “mtu wa hekima na busara” ambaye alisubiria mpaka siku ya mwisho na kumuona Masiha. Leo pia tuna jambo kama hilo, Anna anasifika kwa ujasiri wake, na huduma yake katika hekalu, akisali na kufunga. Alikuwa ni mjane na ilikuwa ni miaka saba tu baada ya kuolewa, na alikuwa akitumikia katika hekalu karibia nusu ya karne moja. Ingawaje angeweza hata kuomba udhuru kwasababu ya umri wake, Anna alijitoa mwenyewe daima katika sala na kufunga. Hakuna sehemu yoyote katika Agano jipya tunasoma kuhusu “nabii Mwanamke” msemaji wa Mungu, ni Anna pekee. 


Aliweza kutambua ujio wa Bwana kwasababu ya kujaliwa neema na Mungu, alitambua ujio wake baada ya kupelekwa hekaluni na Maria na Yosefu. Tunaona uzuri uliopo katika jibu la Anna. “Anaongea kuhusu Mtoto kwa wale wote waliokuwa wakimsubiri mtoto na mkombozi wa Yerusalemu”. Anna anawakilisha waumini wa kweli kwa njia ya sala. Huduma yake kwa hekalu na kutangaza kwake habari njema kuhusu Yesu. 


Tunapata somo kubwa sana kwetu kuhusu kukutana kwake na Yesu. Tunapokutana na Yesu katika maisha yetu ya Imani na sala, je tunapata furaha ya kushirikisha kwa wengine? Pengine kwa njia ya maneno yetu lakini zaidi mara nyingi kwa kuwa mashahidi wake. Ukweli ni kwamba maana halisi ya Noeli inapaswa kushirikishwa kwa wengine. Inapaswa kushirikishwa katika ulimwengu mzima na kutambua ujio wa Masiha ulimwenguni. 


Tafakari, juu ya nabii Anna. Jaribu kufikiria juu ya furaha yake alivyokuwa akimuona huyu Mfalme aliyezaliwa. Sali ili hali kama yake ikupate uweze kumtangaza Kristo kwa maisha yako na kumfanya Mungu awe njia katika njia yako. 


Sala: 

Bwana, ninakuomba niweze kufahamu maana halisi ya Noeli. Ninakuomba niweze kuhifadhi furaha hii ya kuzaliwa kwako katika moyo wangu. Ninakuomba niweze kuishi zaidi kwa makini na katika Imani ninaposhiriki katika mafumbo haya ya Noeli. Yesu nakuamini wewe. 

Amina

Maoni


Ingia utoe maoni