Jumamosi, Disemba 16, 2017
Desemba 16, 2017.
------------------------------------------------
JUMAMOSI, JUMA LA 2 LA MAJILIO
Somo la 1: Ybs 48: 1-4, 9-11 maisha ya Elia yanasifiwa na mwandishi wa Kitabu cha Yoshua Bin Sira. Alihubiri toba, alichukuliwa mbinguni na alikuwa mpatanishi
Wimbo wa katikati: Zab 79: 2-3, 15-16, 18-19; Bwana tunakuomba uso wako utuangaze nasi tutakuwa salama. Tunakuomba utupe uzima nasi tutaliita jina lako.
Injili: Mt 17: 10-13 Yesu, akiongelea kuhusu mapokeo kwamba Elia atakuja tena, Yesu anasema kwamba tayari ameshakuja katika ujio wa Yohane Mbatizaji lakini alikataliwa.
------------------------------------------------
YAHWEH NI MUNGU WETU
Elia alikuwa akitazamiwa kurudi ulimwenguni kabla ya mwisho wa nyakati na kabla ya kuja kwa Masiha. Watu hawakuwa na uhakika. Kama Yohane Mbatizaji alikuwa ndiye Elia ajae ulimwenguni, basi Yesu ni Masiha, anayekuja kipindi cha mwisho cha ulimwengu. Yesu anajibu swali la wafuasi kwamba Yohane Mbatizaji kweli yeye ndiye Elia aliyerudi ulimwenguni.
Kazi ya Yohane Mbatizaji kama Elisha aliyekuja Waandishi walishindwa kuiona. Walishindwa kumuona yeye akitimiza kazi ya Elisha ya kuandaa njia kwa ajili ya Bwana. Kama Yohane alivyokuwa na kazi ya pekee ya kumtambulisha na kuandaa njia kwa ajili ya ujio wa Kristo, sisi pia tuna kazi ya kumkaribisha Yesu daima. Yesu alikuja miaka mingi iliopita, lakini daima anatamani kuja daima katika maisha yetu. Na anaweza kuja tu kama tumejiandaa vizuri.
Ujumbe mkuu wa Yohane ni kutubu dhambi zetu. Ingawaje sisi wote tunakazana kujikinga na dhambi, kwasababu ya matokeo ya kuanguka kwa Mwanadamu, hatupaswi kusahau kwamba wito wetu ni kuwa wakamilifu, kuwa wakamilifu kama Baba yetu wa Mbinguni alivyo mkamilifu. Tunaitwa kutambua dhambi zetu, kuziungama, na kujitahidi kujinasua kutoka kwenye dhambi hizo.
Kipindi cha majilio ni kipindi muhimu cha kufanya hivyo daima, na ni muhimu kutafuta neema zinazopatikana kwa neema ya Sakramenti ya kitubio katika kipindi hiki kitakatifu. Tujitazame wenyewe katika mioyo yetu ni kwa jinsi ghani tulivyo tayari kuihubiria mioyo yetu kuhusu kutubu na kuacha dhambi. Kukubali toba kutubu kipindi hiki ni kitu chema kabisa ambacho twaweza kufanya ili kuandaa kuja kwa Kristo daima katika maisha yetu.
Sala:
Bwana, nisaidie niweze kuziona dhambi zangu kadiri tunavyozama katika kipindi hichi cha majilio. Nisaidie niweze kutambua yale yote yanayonifanya niwe mbali nawe na kuyaacha kwa moyo wote. Yesu nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni