Jumamosi, Disemba 09, 2017
“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba 9, 2017.
------------------------------------------------
JUMAMOSI, JUMA LA 1 LA MAJILIO
Somo la 1: Isa 30:19-21, 23-26 Mungu ni mwingi wa neema kwa wanao mwita, mara anaposikia hukujibu. Mungu ataviunga vidonda vya watu wake na kuponya jeraha walizo umizwa.
Wimbo wa Katikati: Zab 146:1-6 Mungu anaujenga Yerusalemu na kuwarudisha Waisraeli kutoka utumwani. Ataponya mioyo iliovunjika, na kufunga vidonda vyao. Wana heri wanao mtumaini Bwana.
Injili: Mt 9:35 – 10:1,5, 6-8 kwa kuvutwa na huruma ya watu waogonjwa, Yesu anawaamuru mitume wake wachukue kazi yake ya kuponya na kuwafariji watu.
------------------------------------------------
TUMWACHE MUNGU ATUANDIKIE HISTORIA MPYA
Mpango wa Mungu unatusogeza mbele bila kuturudisha nyuma. Tunaweza tu kusogea mbele kwa fadhila au kurudi nyuma kwa kutenda dhambi. Kama hatufanyi ili viendane na Ufaleme wa Mungu basi uwepo wetu hauna maana. Maisha yetu yanakosa utaratibu. Katika Biblia, Mungu ameingia katika maisha ya mwandamu ili kumleta karibu na mapenzi yake. Anatutegemea sisi tuchukue jukumu, kumgeukia na kuchagua njia nyemembamba ambayo haipitwi na wengi na kufuata njia yake ambayo wakati mwingine tunaweza tusiione kama tunavyotaka wenyewe, Neno lake. Huu ndio muda wa kujitakasa-muda ambao tupo jangwani.
Leo katika liturjia yetu ya kipindi cha majilio, tunaomba kwa ujio wa Mwana wa Mungu, tukijua pia alishakuja, tunaye pamoja nasi. Tunatumaini katika kile ambacho yeye anacho. Hatuwezi kutosheka kwakusema hatumuhitaji Yesu kwa uponyaji, huruma yake ya kutugusa. “kwa kuwaona makutano aliwahurumia” na leo hii hatuna sababu ya kusema kwamba huruma yake imeisha kwetu. Anaendelea kuponya mioyo iliyo umizwa na kufunga vidonda vyao. Anauwezo wa kutuambia idadi ya nyota na kuzipa kila moja jina. Injili inatuambia kwamba aliwatuma wale mitume kumi na mbili na kuwapa mamlaka ya kuponya na kuondoa pepo wabaya na kuponya magojwa ya kila aina, “kuponya wagonjwa, kufufua wafu, na kufukuza pepo. Mmepewa bure toeni bure”. Mamlaka haya hayaja ondolewa ndani ya kanisa na watu wake.
Katika somo la kwanza tunasikia pia: “hata ugeuke kushoto au kulia au nyumba utasikia sauti ikikuambia “Njia ni hii ifuate”. Nabii anawapa uhakika watu kwamba kama watamtafuta Mungu kwa hakika watampata-njia ni hii ifuate”!. Mpaka tuisikia hiyo sauti na kuifuata, hatuwezi kuwa huru mpaka tumeifuata sauti hiyo. Ni kitendo cha kubadili mtazamo wetu na kuchagua kuyafuata mapenzi ya Mungu, bila kujali gharama yake! Sisi sote tunafanya makosa katika maisha. Wengi wetu tunapoteza mwelekeo tukiwa njiani. Tunapaswa kurudi na kusikiliza sauti ya Mungu ndani mwetu. Wakati Mungu anatamani kuingia katika maisha yetu, tunapaswa kufanya njia iwe imenyooka ili yeye aweze kuingia ndani.
Sala
Mungu mwenye huruma, tunaomba Ekaristi tunayopokea na liturjia tunayo adhimisha ituletee msaada wa neema yako, tuweke huru kutoka katika dhambi zetu, na utuandae kwa kuzaliwa kwa Mkombozi wetu. Yesu nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni