Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Septemba 30, 2017

Jumamosi, Septemba 30, 2017.
Juma la 25 la Mwaka

Kumbukumbu ya Mt. Jerome, Mwalimu wa Kanisa

Zek 2: 5-9, 14-15;
Yer 31: 10-12, 13;
Lk 9: 43-45


ROHO MTAKATIFU ANAFUMBUA MAFUMBO YA IMANI!

Yesu katika Injili anongea kuhusu kifo chake. Lakini wanafunzi wake hawaelewi mafumbo haya makuu. “Walishindwa kufahamu ana maanisha nini lakini wakaogopa kumuuliza nini maana ya msemo huo” . Lakini Yesu hakuumizwa na hali yao ya kutokuelewa. Alifahamu kwamba hawata elewa mara moja. Lakini hili halikumzuia kuacha kuwaambia. Kwasababu alitambua muda utafika tuu watakuja kuelewa tu. Wataelewa haya wakati Roho Mtakatifu atakapo washukia na kuwaambia kweli yote. Hii ni kazi ya Roho Mtakatifu ili kuelewa haya mafumbo makuu.

Ni kweli pia kwa upande wetu. Tunapokumbana na mafumbo haya ya mateso ya Yesu, na wakati tunapo kumbana na mateso yetu wenyewe au mateso ya wale tunao wapenda, tunaweza tuka changanyikiwa kwanza. Tunahitaji zawadi ya Roho Mtakatifu ili tuweze kuelewa mafumbo haya. Mateso hayakwepeki. Sisi wote tunavumilia mateso. Na kama hatutamrushusu Roho Mtakatifu atembee katika maisha yetu tutaishi katika kuchanganyikiwa na kuwa na mashaka daima. Lakini kama tukimruhusu Roho Mtakatifu afungue akili zetu, tutaanza kuelewa ni kwa jinsi gani Mungu anafanya katika katika maisha yetu katika mateso yetu, kama alivyo leta ukombozi ulimwenguni kwa njia ya mateso, kifo na ufufuko wa Kristo.

Je, unataka Roho Mtakatifu akufunulie maana na thamani ya mateso katika maisha yako? Sali kwa Roho Mtakatifu ukimuomba neema na umwache Mungu akuongoze katika chemchemi ya mafumbo haya ya Imani.

Leo, tunasherekea kumbukumbu ya Mt. Jerome, ambaye anajulikana kama Baba wa elimu ya sayanzi ya Biblia, ni yeye aliye tafsiri Agano la Kale la Kiebrania na Agano Jipya la Kigiriki kwenda katika lugha ya Kilatini. Alisema kwamba; “ujinga wa kutokufahamu maandiko, ni ujinga wa kutokumfahamu Kristo”.

Sala:
Bwana, ninatambua kuwa uliteseka na ukafa kwa ajili ya wokovu wangu. Ninatambua mateso yangu yanaweza kuleta maana mpya katika msalaba wako. Nisaidie niweze kufahamu mafumbo haya makuu niweze kufahamu thamani kubwa katika msalaba wako na wangu pia. Yesu, ninakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni