Ruka hadi maudhui
Mkatoliki Leo
Tafakari

Mungu Ana Mpango Nasi!

· na Shajara Administrator

Masomo ya siku hii Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bikira Maria → Mik 5:1-4 · Zab 13:5-6 · Mt 1:1-16, 18-23
Bikira Maria Mama yetu, alichukuliwa mimba kitakatifu, alizaliwa na kuishi bila dhambi, na sasa anatuombea ili hata mmoja wetu asipotee. Sisi, wanawe tunafurahi kusheherekea sikukuu yake ya kuzaliwa. Kuhusu sikukuu ya leo Mt. Andrea wa Crete anasema,"viumbe vyote vilivyo umbwa viimbe sifa na kucheza na kwa pamoja viungane kuadhimisha utukufu wa siku hii...kwani leo hekalu limejengwa kwa ajili ya Muumba wa ulimwengu". Maria alizaliwa kama hekalu la Muumba, na kwa njia ya utii wake akatimiza lengo lake ambalo alizaliwa kwa ajili yalo.

Kama Mungu alivyokuwa na mpango kwa Maria, kuzaliwa kwetu sio kwa bahati mbaya au makosa. Mungu ana mpango nasi. Kama Maria alivyotimiza lengo lake duniani, tunapaswa kutambua lengo letu katika maisha na kuwa waaminifu kwa lengo hilo. Tunapaswa kuheshimu maisha ya wengine pia, kwani Mungu naye ana mpango nao pia! Tuwaombee kwa namna ya pekee “ watoto wa kike” ambao siku hii pia ni maalumu kwa ajili yao pia

Sala:
Salamu Maria uliye jaa neema Bwana yu nawe umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzawa wa tumbo lako amebarikiwa, Maria Mtakatifu Mama wa Mungu tuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu.
Amina.
0 Maoni
WhatsApp Facebook

Maoni (0)

Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.

Ingia utoe maoni