Jumapili, Machi 19, 2017
Jumapili, Machi 19, 2017.
Juma la 3 la Kwaresima
Kut 17: 3-7;
Zab 95: 1-2, 6-9;
Rum 5: 1-2, 5-8;
Yn 4: 5-42.
UNA KIU?
“Gods must be crazy” Ni jina la filamu na ni juu ya watu walioko katika Jangwa la Kalahari. Filamu hii inaonesha wazoefu wa jangwa. Mmoja wa watu hawa alitembelea mabubujiko ya maji ya Tungela (maporomoko makubwa ya maji Afrika), huko Afrika kusini. Alishangazwa kuona maji makubwa yanashuka kutoka juu. Alisimama pale kwa masaa akishangaa. Hawa watu waliopo Kalahari walizoea kukusanya maji kutoka katika majani (umande) au kupata maji kutoka katika aina ya mmea ambao shina lake huwa na maji, ili kupooza kiu yao. Kama ilivyo katika simulizi hilo, lirtujia ya leo ya Domini ya tatu ya Kwaresima inatuonesha kwamba sisi wote tuna kiu. Watu wana kiu ya fedha, anasa, madaraka, na mali, na hata kama akipata nyingi, bado kiu ni kubwa. Katika hali nyingine kuna “maji ya uzima” upande mwingine ndani ya Yesu Kristo. Tunapojiandaa wenyewe kuingia katika mafumbo ya mateso, kifo na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo kipindi hiki cha Kwaresima, tunaitwa leo tutulize kiu yetu ya kiroho na kutuliza kiu ya Yesu anayezitafuta roho zetu na ana zisubiri zirudi kwake. Yesu alipata kiu ya mwanadamu kumrudia Mungu, na hivyo akasema pale msalabani “Nina kiu”.
Katika somo la kwanza tunaona Waisraeli wanao lalamika. Watu hawa hawa waliovushwa salama kutoka katika utumwani huko Misri, na waliokuwa wakitembea kwa uhuru kuelekea Nchi ya ahadi. Kwanza kabisa walilalamika kuhusu chakula, Mungu akawapa mana, mkate kutoka mbinguni. Hata baada ya kuona muujiza huu bado hawaja uamini upendo wa Mungu. Wakaanza kukusanya zaidi ya mahitaji yao, lakini yote iliharibika siku iliofuata. Alafu wakaanza kulalamika kwasababu ya maji. Pamoja na hilo Mungu akafanya muujiza mwingine akawapa maji. Lakini Israeli hakujifunza kumtuminia Mungu. Mwanadamu ni kiumbea ambaye haridhiki. Mahitaji yetu daima tunaona hayatoshi, yanaendelea kuongezeka daima. Ni kama vile kula chumvi, unahisi kiu kila wakati, alafu baadae unakula tena chumvi unahisi kiu tena.
Katika somo la Injili tunamuona huyu Mwanamke msamaria ambaye pia alikuwa akiishi maisha yake yasio pendeza. Alikuwa katika kisima ili kutuliza kiu yake ya kila siku. Alikuwa anajiribu kutuliza kiu ya mwili wake kwa kila aina ya anasa. Lakini kila siku alikuwa akirudi katika kisima kwa ajili ya maji. Yeye kama ilivyo kwa wanadamu wote ni lazima alisimama nakuuliza “hivi kuna aina ya maji ambayo nikinywa sintaona kiu tena?”. Mt. Agustino anatoa jibu anavyosema “mioyo yetu haitatulia …hadi itakapo tulia kwako Bwana Yesu”
Yesu alikuwa njiani kuelekea Yerusalemu kwa kupitia Samaria. Watu wasamaria walionekana kama Wayahudi wasio faa au Wayahudi waliochanganyika. Hawakuwa wakichukuliwa kama sehemu ya jamii ya Wayahudi. Hata tunaona Yesu anakutana na Mwanamke Msamaria. Huyu Mwanamke alikuja katika kisima kuja kuchota maji saa sita mchana. Hii ilikuwa sio kawaida kwasababu, wanawake walikuja kuchota maji wakiwa katika makundi tena ikiwa ni hasubuhi au jioni. Huyu mwanamke inaonekana alipenda kuwakwepa wenzake pengine kwasababu ya tabia ya maisha yake ambayo Yesu alimwambia baadae. Yesu akiwa ni Myahudi anamuomba maji ya kunywa. Alikuwa na mazunguzo naye ambayo yalimlenga kutoka katika mazungumzo ya maji ya kawaida hadi kwenye maji ya uzima, kutoka katika kiu ya kidunia hadi kiu ya kiroho. Anashindwa kumtambua Yesu hapo mwanzo, na Yesu anirarua dhamiri yake kwa kufunua ukweli wa maisha yake. Hili lilikuwa rahisi kwake kupokea neema ya Mungu. Yesu anamsaidia katika hali ya kukuwa na kutambua kumwadudu na hapo anamtambua Yesu kama Masiha. Baada ya kumtabua Yesu, analeta kijiji kizima kwake. Mwanamke ambaye alikuwa amekataliwa na jamii anakuwa chombo cha Mungu cha kuwaleta wanakijiji kwa Yesu. Alikuja kuchukua maji ya kawaida akarudi na maji ya uzima. Yesu hakunywa hata tone moja la maji, lakini kiu yake ilitulizwa kwa kupata roho moja kwa ajili yake.
Yesu alijua yote kuhusu huyu Mwanamke lakini alitaka kumpa maji ya uzima. Alitaka kuzima kiu ambayo yeye alikuwa nayo rohoni mwake. Alivyokuwa akiongea naye, na kuanza kumsikiliza kiu yake ilianza kuzimwa. Ilianza kuzimwa kwasababu ndicho alichohitaji, tunachohitaji wote, ni upendo huu kamili na kukubaliwa na Yesu, ambao Yesu anautoa mwenyewe. Alitoa kwake, na anataka kuutoa kwetu pia. Cha kushangaza Mama huyu aliondoka na kuacha “mtungi”. Hakuchukua maji aliokuwa amekuja kuchukua. Au alichukuwa? Katika hali hii ya kuacha mtungi ni alama kwamba kiu yake ilikuwa imezimwa kwa kukutana na Yesu. Hakuwa tena na kiu, Yesu alizima kiu yake.
Katika kuishi kwetu kila siku, tunajikuta tukimwacha Mungu na kutafuta mambo yanayo pita. Tunafatilia tukitafuta maana katika hivyo vitu lakini tunakuta hamna, ni utupu ndani yake. Tutafakari juu ya kiu isiopingika tulio nayo ndani mwetu. Tukisha itambua, tuelekeze dhamiri zetu kumwelekea Yesu ili azime kiu yetu kwa maji ya uzima. Tukifanya hivi, tutaacha mitungi mingi ambayo kwakweli haizimi kiu yetu.
Sala: Bwana, wewe ni maji ya uzima ambayo roho yangu inatafuta. Ninakuomba nikutane na wewe katika maisha yangu, katika aibu yangu na maumivu ya moyo. Ninaomba nikutane na upendo wako, upole wako na kukukubali sasa, ninaomba upendo wako uwe chanzo cha maisha yangu ndani yako. Yesu nakuamini wewe. Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni