Ruka hadi maudhui
Mkatoliki Leo
Tafakari

Jina Takatifu la Yesu

· na Shajara Administrator

Masomo ya siku hii Jumatano ya 7 ya Mwaka → Ybs 4:11-19 · Zab 119:165, 168,171-172, 174-175 · Mk 9:38-40
Katika Injili tunaona mtu wakitoa pepo kwa jina la Yesu. Hakuwa mmoja wao wa wale wafuasi wa Yesu, kwahiyo wafuasi wa Yesu, walitaka kumzuia. Yesu anawaambia kama anafanya vizuri, akitenda ishara na miujiza, akiwafukuza pepo kwa jina lake, hawezi kamwe kufanya kitu kinyume chake. Watu sasa wame pokea mamlaka ya Yesu juu ya viumbe vyote, juu ya pepo wachafu na hata mamlaka juu ya kifo. Jina la Yesu ni jina lenye nguvu, ambalo haliwezi kufananishwa au kubadilishwa na jina lingine. “hakuna jina jingine, chini ya mbingu tulilopewa wanadamu ambalo tunapaswa kuokolewa nalo” (Mdo 4:26). Wakati wa kipindi cha Yesu tunaona jina la Yesu likifanya maajabu na miujiza, na linaendelea hata leo. Yesu maana yake “Anaye komboa” ukombozi unatolewa naye kwaajili yetu wote. Wote wanaokubali jina la Yesu na kumfanya Bwana wa maisha yao, wanaweka mipango yao kwake, kwasababu jina la Yesu lilifunua mipango mipya kwa wafuasi wake.

Sala:
Bwana naomba jina lako litukuzwe ndani yangu na kupita mimi.
Amina.
0 Maoni
WhatsApp Facebook

Maoni (0)

Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.

Ingia utoe maoni